April 21, 2017

SERENGETI BOYS MBELE YA GABON LEO


SERENGETI-BOYS-SA
Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kesho Jumamosi inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gabon katika Viwanja vya Shirikisho la Soka Morocco (FRMF) nchini Morocco.
Serengeti Boys inajiandaa na fainali za mataifa Afrika kwa vijana zinazotarajiwa kuanza Mei 14, mwaka huu nchini Gabon ambapo wamepangwa Kundi B sambamba na Niger, Angola na Ethiopia.
Akizungumza kutoka kambini nchini Morocco, Shime alisema lengo la mchezo huo ni kuangalia mapungufu ya kikosi chake kabla ya kulekea nchini  Gabon tayari kwa mashindano hayo.
“Tunashukuru maandalizi yapo vizuri na kila kitu kipo sawa, vijana wako na ari kubwa kabisa na wako tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Gabon ambao ndiyo  wenyeji wa michuano hiyo, naamini itatusaidia kujua aina ya timu tunazoenda kucheza nazo, hivyo kwetu ni jambo zuri.
“Hii mechi itasaidia kutambua mapungufu ya wachezaji wangu kabla ya kurudiana nao Aprili 25 kwa sababu baada ya kucheza na Ghana nyumbani hatukucheza mchezo wowote,” alisema Shime

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE