April 27, 2017

SABABU YA KUKAMATWA DKT JESCA MSAMBATAVANGU ZAANIKWA

ALIYEKUWA mwenyekiti wa wa chama cha
mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa aliyefukuzwa
chama hicho kwa usaliti wakati wa uchaguzi
mkuu mwaka 2015 Dkt Jesca Msambatavangu (pichani)amekamatwa na jeshi la polisi kwa
tuhuma za kumvamia mwanamke mmoja na
kumfanyia vitendo vya kinyama ikiwa ni pamoja na kumchoma sindano inayodhaniwa kuwa na sumu.


Kamanda wa polisi wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi amezungumza na mtandao wa matukiodaimaBlog   kwa njia ya simu jana kuwa Dkt
Msambatavangu alikamatwa jana mchana na anashikiliwa na jeshi hilo kabla ya kufikishwa mahakamani .

“ Ni kweli tunamshikilia Jesca Msambatavangu
kwa tuhuma za kumvamia na kumpiga mwanamke mmoja wa kibwabwa katika Manispaa ya Iringa …walimuumiza sana na walimchoma
sindano inayodhaniwa kuwa na sumu “

Kamanda Mjengi alisema kuwa mwanamke
huyo jina limehifadhiwa alivamiwa na watu
wanne akiwemo Msambatavangu na kuwa bado
jeshi la polisi linaendelea na msako mkali wa
kuwasaka watuhumiwa watatu majina yao
yamehifadhiwa waliohusika katika tukio hilo .

Hata hivyo alisema wanaendelea na msako huo
wa kusaka watu hao walioshiriki popote walipo
ili kufikishwa mahakamani na kuonya kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwataka wananchi wa
mkoa wa Iringa kutoa ushirikiano wa kuwafichua wote wanaojihusisha na matukio yote yasiyo faa katika jamii .

Dkt Msambatavangu toka afukuzwe na chama
chake katika vikao vyake mjini Dodoma na toka afukuzwe amepata kusikika kupitia kituo
Kimoja cha radio  mkoani Iringa kuwa kwa
sasa hatataka kujihusisha na shughuli ya siasa tena na kuwa yote yaliyotendeka ndani ya chama chake amemwachia Mungu

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE