April 10, 2017

ROMA MKATOLIKI AFUNGUKA TAZAMA HAPA ALICHOSEMA

>
 Roma Mkatoliki akizungumza na vyombo vya habari

Msanii Roma Mkatoliki asema anahofia maisha yake siku moja tu baada ya kupatikana katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Akizungumza na vyombo vya habari akiwa na waziri wa habari, utamaduni ,sanaa na michezo Dkt  Mwakyembe , msanii huyo ameelezea vile walivyotekwa siku ya Jumatano na kufungwa pingu na kitambaa usoni na baadaye kusafirishwa hadi eneo wasilolijua.

Akizungumza na hisia na uchungu mwingi Roma alisema kuwa walipofikishwa walipopelekwa walipata mateso mengi kwa kupigwa hadi siku ya Ijumaa usiku.

Roma Mkatoliki: Tukatolewa tulimokuwepo siku ya ijumaa jioni tuliwa tumefungwa uso, na mikono na miguu. Tukapelekwa sehemu tukatupwa kwenye dimbwi la maji karibu na baharini Roma anasema kuwa alipata fahamu na kuweza kuwafungua wenzake na kutembea mwendo mrefu ambapo walifika katika maeneo ya ununio.

Hata hivyo msanii huyo alishindwa kuelezea baadhi ya maswali aliyoulizwa kuhusu mahojiano na waliowateka huku akisema tu kwamba tayari wamewasilisha malalmishi yao kwa polisi kwa ucunguzi.

Tutakupasha zaidi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE