April 24, 2017

RC, IRINGA ATUMA SALAM ZA POLE KWA MKUU WA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA

 .......................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog 
MKUU  wa mkoa  wa Iringa  Amina Masenza amewatembelea askari watatu kati ya  wanne  wa  kikosi cha  zimamoto na uokoaji  Manispaa ya  Iringa  ambao  walipata ajali  ya  gari jana  usiku   wakati  wakielekea kuzima moto  kijiji cha Mkungugu .

Akizungumza na  majeruhi  watatu  ambao  wameruhusiwa  leo  kutoka katika  Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa  ambako  walilazwa  kwa matibabu ,mkuu wa  mkoa  alisema  amepokea kwa  masikitiko makubwa juu ya ajali  hiyo na  kuwa bado  anamshukuru  Mungu kwa  kuwaepusha  salama katika ajali  hiyo.

 Masenza  alisema kazi  ambayo askari  hao  walikuwa  wakienda  kuifanya ni kazi ya  kuokoa maisha na mali  ya mkazi mmoja wa  Mkungugu  ambae  nyumba  yake  ilikuwa  ikiwaka moto majira ya saa 7 usiku  hivyo baada ya  kuomba msaada wa  gari la  zimamoto  askari  hao waliondoka  kwa mwendo mkali ili  kufika kwa wakati  kunusuru nyumba na uhai wa  familia  iliyokuwepo ndani ya  nyumba hiyo.

Pamoja na  kuwapa pole  askari  hao  waliojeruhiwa ambao kwa jumla yao walikuwa ni askari watano na kati yao  mmoja aliruhusiwa jana na   watatu  wameruhusiwa  leo huku mmoja akinusurika ,bado mkuu  huyo wa  mkoa alimpa  pole kamanda wa  kikosi  cha Zimamoto na uokoaji mkoa  wa Iringa Keneth Komba kwa askari  wake  kupata  ajali .

Mkuu  huyo wa  mkoa alisema tayari  ofisi yake  imekwisha  shughulikia  suala la  kuvuta  gari  hilo  kutoka  eneo la tukio ili  kuleta  mjini Iringa kwa matengenezo kwani  alisema gari  hilo  ni pekee  mkoa wa Iringa hivyo bila  kulifanyia matengenezo ni hatari kwa  usalama wa mkoa iwapo moto utatokea .

Pia  mkuu   huyo wa  mkoa amempongeza mkurugenzi wa kampuni ya  Tawakali  kwa kuonyesha  uzalendo  wa hali ya  juu kwa kujitolea  gari la kwenda  kuvuta gari  hilo la Zimamoto na uokozi ambalo  lilipata ajali  


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE