April 11, 2017

RC IRINGA AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAZI NZURI YA KUWATUMIKIA WANANCHI

Waziri  wa ardhi  nyumba na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi akisalimiana na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo  alipowasili  ukumbi wa siasa ni  Kilimo mjini Iringa  kufungua mkutano wa uhifadhi wa ikolojia mto  Ruaha mkuu
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akisama taaarifa ya  mkoa
Mkuu  wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akisalimiana na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Jamuhuri Wiliam  akisalimiana na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Waziri  Lukuvi akifurahi jambo na viongozi  wenzake
Mawaziri  mbali mbali  wakimsubiri  makamu wa Rais
Mkuu  wa mkoa wa Njombe Christopher Ole  Sendeka akisalimiana na makamu  wa rais
Makamu  wa  Rais  akisalimiana na mbunge wa Mbeya
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah kulia   akisalimiana na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Waziri wa mazingira na muungano Januari Makamba akizungumza katika kikao hicho
MKUU  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kwa kazi nzuri inayofanya katika kuwahudumia Watanzania.
 
Mkuu  huyo wa mkoa ametoa pongezi hizo leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati akimkaribisha makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa kwanza wa uhifadhi wa Ikolojia ya mto Ruaha mkuu ,
Alisema  kuwa watanzania wanaimani na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Dr. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo hivyo wao kama  viongozi kazi yao  kubwa ni  kufanya kazi kwa kasi zaidi  ili  kutokwamisha utendaji kazi wa  serikali.
  
Akielezea kuhusu hali ya chakula kwa msimu wa 2016/17 alisema kuwa matarajio ni mazuri kwani pamoja na mvua kuchelewa kidogo lakini imenyesha vizuri, hivyo ni matarajio wananchi watavuna vizuri, watapata chakula cha kutosha na cha ziada.
 
"Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa wadau wa Mto Ruaha Mkuu ambao ni mhimili mkubwa wa uchumi katika Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla. Pamoja na kwamba mto huu unamchango mkubwa kiuchumi, umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali"
Miongoni mwa changamoto hizo ni vyanzo vya maji kuharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia nchi.
 
Aidha  alisema kuwa madhara yatokanayo na changamoto hizi ni pamoja na wanyama kufa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kina cha maji kupungua katika Mabwawa ya  Mtera na Kidatu na hivyo kusababisha uzalishaji wa umeme kuwa kidogo. 
 "Tunashukuru kwa kikao hiki cha leo na ni matarajio yetu kwamba kitapitia changamoto zilizopo na kuziwekea njia za utatuzi, hatimae kuufanya Mto Ruaha utiririke Mwaka mzima ili kunusuru uhai wa Hifadhi ya Taifa Ruaha na kuimarisha shughuli za kiuchumi. "
Alisema mkuu  huyo wa mkoa  kuwa tayari waliwahi kukaa vikao kadhaa, miaka ya nyuma lakini havikuzaa matunda tuliyokuwa tukitarajia.
Kwani kila sekta imeendelea kuamua kile inachodhani ni kipaumbele bila kushirikisha sekta nyingine, maamuzi ambayo pia yamepelekea ama kupungua kwa maji au kukauka kwa Mto, kutokana na kukosekana mipango thabiti ya matumizi endelevu ya rasilimali maji.
 
''Kufanyika kwa kikao hiki, naamini ni suluhisho la tatizo la kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu''

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE