April 11, 2017

PUMZIKA KWA AMANI ZAHARA NIMEGEUZA NJIANI JIONI YA LEO NIKIJIPANGA KUJA KESHO KUKUONA,

R.I.P ZAHARA MWANA IRINGA 
Dadangu umeishi miaka mingi bila kuugua ugua ovyo,tumekaa nyumba moja kwa upendo mkubwa sana,ulikuwa kama dada yangu wa kuzaliwa toka nimefika Iringa hapa! Mwezi uliopita ukaanza kusumbuliwa na vidonda vya tumbo,toka homa imekuingia haijakuachia hadi leo hii mauti ilipokufika!

Umeondoka mapema sana,ewaacha watoto wadogo Zai, Regina na Rachel! 

Hakika kifo bado kinazidi kutuumiza na kutuliza kila wakati,ndipo kila wakati katika matukio haya nakumbuka lile neno lisemalo "Mwanadam aliezaliwa na mwanamke siki zake si nyingi" hakika hatuna cha kusema zaidi ya kusema kazi yake Mola haina makosa! Bwana alitoa na Bwana ametwaa!

Pumzika kwa amani dadangu Zahara kirangi ni leo majira ya saa 11.09 rafiki yangu kanikuta eneo la M.R Hoteli nikiwa na pilika za kutuma gazetini habari ya makamu wa Rais leo Iringa nilifuatwa na kusalimiwa kisha kuelezwa kuwa Zapara Kilangi umelazwa wodi namba nani Hospitali ya mkoa wa Iringa nikiwa nimeongozana na rafiki yangu kabla ya kufika kituo cha mafuta cha Hope alinieleza hata nikienda kumwona siwezi kuongea nae kwani yu tambani hapo ndipo nilipobadili mawazo kuwa niende kesho asubuhi 

Kumbe kusita kwangu ndio nimemkosa kumpa mkono wa kwaheri namkumbuka Kama dadangu akiwa mtumishi wa ofisi ya Papu akiniuzia vocha akicheka nami ila kaondoka bila kuona tabasamu Lake kweli nenda dadangu wote tutakuja

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE