April 5, 2017

"MUBASHARA"MKUTANO WA WADAU LIPULI FC NA MKUU WA MKOA WA IRINGA UKUMBI WA KRELUU

Mkutano wa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na wadau wa soka mkoa wa Iringa unaendelea muda huu katika ukumbi wa chuo cha Kreluu huku wadau wa Lipuli FC wakiwataja viongozi wa soka mkoa wa Irina na baadhi yao kutoka TFF kuwa ni chanzo cha mgogoro huo .

Katika kikao hicho baadhi ya wanachama wamemtaja mmoja kati ya mtumishi wa umma kuwa amekuwa akitumia ofisi ya umma kupindisha barua mbali mbali za serikali kwa faida yake. 

Hivyo wataka mkutano mkuu wa uchaguzi kuitwishwa ili kumaliza mgogoro huo na kuwa viongozi wenye taaluma watatakiwa kugombea nafasi hiyo iliyopelekea kutengeneza wanachama hewa ili kubadili katiba kutoka mfumo wa wanachama ili kwenda mfumo wa hisa ili watu wajinufaishe. 

Pia wanachama hao wamefichua mbinu ovu za kumfungia aliyekuwa mwenyekiti wao Abuu Changawa Majeck ili wao kuweza kupitisha uovu wao dhidi ya Lipuli FC 

Kuwa kuna njama ya kukopa pesa mamilioni ili kugawana na kuwa yupo tayari kwenda benki kufunga akaunti ya Lipuli fc

ANDONDILE 

Ataja orodha ya viongozi wanaochochea mgogoro Lipuli FC ambao wapo wanne Tff taifa mmoja na wengine watatu ambao amekabidhi majina hayo kwa mkuu wa mkoa Iringa kupelekwa kwa waziri ama kwa Rais


Inaendelea endelea kubaki haha....... 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE