April 5, 2017

MKURUNGENZI MKUU WA NIDA APONGEZA MKOA WA IRINGA KWA KUFANYA VIZURI ZOEZI LA VITAMBULISHO VYA KITAIFA, ASEMA MIKOPO NA TASAF BILA KITAMBULISHO MWISHO

Mkuu wa  Iringa Amina Masenza  akimkabidhi  kitambulisho  cha urai mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Jamhuri  Wiliam leo  wakati wa  uzinduzi  wa zoezi  hilo kwa  mkoa wa Iringa  liilofanyika wilayani Mufindi
Mkurugenzi  mkuu  wa mamlaka  ya vitambulisho  vya  Taifa  (NIDA) Andrew Massawe  akitoa  maelezo ya kuanzishwa kwa  zoezi  hilo
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akiwahutubia wananchi wa  Mji wa Mafinga  wilaya ya  Mufindi  leo wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya NIDA
r;">
Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Jamhuri  wiliam akitoa  taarifa  ya zoezi hilo wilayani kwake
Wakazi wa  Mafnga  wakipiga  picha kwa  ajili ya vitambulisho vya NIDA
Mkuu  wa mkoa wa Iringa  Amina Masenza  akitembelea banda la  NIDA  kuona  zoezi la  uandaaji wa  vitambulisho  vya NIDA
kaimu mkurugenzi wa NIDA Alphonce  Malibicha  kushoto  akionyesha aina ya  kitambulisho cha NIDA kwa  mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  kulia na anayefuata  ni mkurugenzi mkuu wa NIDA Taifa  Andrew Massawe na mkuu wa wilaya ya  Mufindi Jamhuri  Wiliam
Vitambulisho  vya  NIDA  kwa  ajii ya  wakazi wa Mufindi  vikiwa tayari
Wananchi  wakiwa katika  uzinduzi wa vitambulisho vya  NIDA  leo
Mkazi wa Mafinga  akifurahia  kukabidhiwa  kitambulisho cha Taifa
Aliyekuwa  mkuu wa wilaya ya Makete Daud Yassin akikabidhiwa  kitambulisho cha Taifa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  leo
Na MatukiodaimaBLOG
MKURUGENZI mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa ( NIDA) Andrew Massawe amepongeza zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kitaifa mkoani hapa na kuwa mara baada ya zoezi hilo kukamilika hakuna mtu atakayepata mkopo au kusaidiwa na TASAF bila kitambulisho hicho.

Akizungumza jana wakati akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kuzindua zoezi hilo kimkoa katika uwanja wa Mashujaa Mafinga wilayani Mufindi alisema mkoa wa Iringa umeanza vizuri zoezi hilo na ni matumaini ndani ya siku 60 walizotoa zitatosha kutoa vitambulisho kwa wananchi wote.

" Huu ni  mkoa  wa kwanza  Tanzania  kufanya  jambo   kubwa kama  hili  ......mamlaka  ya  vitambulisho vya  Taifa  imlenga  kuwaandikisha  Raia  wote  wenye miaka kuanzia 18 na kuendelea  wakiwemo  wahamiaji  ambao  wanaishi hapa  nchini kwa  kufuata  taratibu zote "

Alisema  kuwa   zoezi hilo  lina tija   kubwa kwa  usalama wa watanzania  na  kuwa  linaendeshwa  kwa  kushirikiana na iadara  mbali mbali  ikiwemo ya  uhamiaji  na Tamisemi   kuwa  lengo la  kuwashirikisha  Tamisemi ni  kuweza  kuthibitisha uraia wa raia  na Rita  kwa  ajili ya  kuthibitisha umri wa m husika na uhamiaji  kwa ajili ya  kuthibitisha  uraia wa  mhusika .


Mkurugenzi  huyo  alisema  zoezi hilo linafanywa kwa mujibu wa sheria namba 11 ya mwaka 1986  iliyofanyiwa marekebishwa  mwaka  2012 na kimsingi  kazi ya uandikishaji wa  watu lilianza Octoba 3 mwaka  2016  na mkoa  wa Iringa umefanya  vizuri  sana katika  kukamilisha  zoezi la uhakiki na ukamilishaji wa  uandikishaji wa  watumishi wa umma.


Hata   hivyo  alisema  tayari  wamekubaliana na TASAF  katika uendelea  kuwasaidia wananchi  wanaotoka kaya masikini zisizo na uwezo  hawatamsaidia  mtu  yeyote  ambaye hana  kitambulisho cha uraia  pia taasisi  za  kifedha  zinazotoa  mikopo  hasitatoa  mikopo kwa  mtu  yeyote asiye na kitambulisho  cha NIDA

Akiwahutubia  wananchi hao mkuu wa mkoa wa Iringa alisema  kuwa baada ya kuona mafanikio makubwa katika zoezi la
usajili wa Watumishi wa Umma na Wananchi wa Wilaya ya Mundi
lililofanyika, Uongozi wa wa  mkoa walikubaliana , kila Wilaya katika siku 60
zijazo kuhakikisha kuwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na
kuendelea wawe wametambuliwa na kusajiliwa. 

 
"Jukumu hili ni la Viongozi wote kuanzia Wakuu wa Wilaya, Makatibu
Tawala, Wakurugenzi kwenye Halmashauri zote, Kamati za Ulinzi na
Usalama, Waheshimiwa Madiwani, Watendaji Kata, Watendaji wa Mitaa
na Vijiji."

Alisema  kuwa anatambua kuwa katika Wilaya wanamipango mingi ya kutekeleza lakini kama
Mkoa kwa sasa kipaumbele kikubwa ni kutekeleza agizo la kitaifa   la serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt John Magufuli  kuhakikisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanasajiliwa na kupata
Vitambulisho vya Taifa  wakiwemo Wageni wote wanaoishi kihalali
kwenye Mkoa wetu.

"Serikali imeshaelekeza  na kama sote tunavyotambua umuhimu wa zoezi
hili kwa Taifa, hatuna budi kutekeleza kwa vitendo.hivyo tuonyeshe ari,
moyo wa kujituma na tufanye kazi kwa mshikamano kama viongozi
katika kulifanikisha hili, ili mkoa wetu uendelee kuongoza katika
kufanikisha maagizo ya Serikali"
Kuwa faida za kukamilisha zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu
katika mkoa wa Iringa ni kuwa na Kitambulisho cha Taifa kutawapunguzia kutembea na utitiri wa
kadi, kuwawezesha wananchi kupata mikopo kirahisi katika taasisi za
fedha, kuwasaidia wananchi kutambulika kirahisi kupata huduma za
maendeleo mfano kuwatambua wanufaika halisi kaya Masikini zenye
kuhitaji msaada wa TASAF, usajili namba za simu  na  huduma nyingine 
.
"Niwaombe sana ndugu wananchi kwa faida nyingi na pana za
vitambulisho hivi, kila mmoja wenu akawe balozi wa mwingine na
kuhakikisha wananchi wote wa Iringa mnajitokeza kwa wingi kusajiliwa.
Na wale mtakao bahatika kupata Vitambulisho vya Taifa mvitunze na
kuvitumia vizuri kama ilivyokusudiwa."
Hivyo alisema wito wake  kwa Viongozi wa Kisiasa, Madhehebu ya Dini
Ndugu Wananchi; suala la Vitambusho vya Taifa halina chama, wala
dini  zoezi la Kitaifa na ni kwa manufaa ya kila raia  lazima kila mmoja kulichangamkia .


"Nichukue fursa hii kuwasihi na kuwaomba sana viongozi wa Dini na siasa
tushikamane na kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wananchi tunao
waongoza wanapata taarifa sahihi na kwa wakati, na wanajitokeza kwa
wingi kusajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa...Pamoja na kila mwananchi kushiriki; lazima tuwafundishe wananchi wetu kuwa wazalendo katika zoezi hili kwa kuhakikisha wana wachua wale
wote ambao watakosa sifa za uraia kupenya na kupewa Vitambulisho vya
Taifa"

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE