April 12, 2017

SERIKALI TUSAIDIENI KUNUSURU MTO RUAHA MKUU - DKT KIJAZI


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbali mbali wakitazama mto Ruaha mkuu unavyokauka leo kutoka kushoto Mkurugenzi wa TANAPA Dkt Allan Kijazi, waziri wa ardhi, nyumba na makazi William Lukuvi na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza 
Waziri Lukuvi akimwonyesha makamu wa Rais kiboko 
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa Dkt Allan Kijazi akionyesha jinsi mto Ruaha mkuu unavyo kauka mbele ya makamu wa Rais 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Kushoto na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi leo wakati wa kutembelea eneo la mradi wa ikolojia mto Ruaha mkuu leo kushoto mwenye miwani ni waziri wa mazingira na muungano January Makamba 
Mwanahabari Tukuswiga Mwaisumbe ambae katibu wa IPC akitazama Ikolojia ya mto Ruaha mkuu 
Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Ayubu Wamoja akitazama mradi wa hifadhi ya Ikolojia mto Ruaha mkuu leo 
Waziri wa mazingira na Muungano January Makamba akitazama mto Ruaha mkuu leo 
Mwanahabari Adam Mzee kutoka ofisi ya makamu wa Rais kulia akiwa na mzee wa matukiodaima leo 

Na Matukodaimablog

MKURUGENZI mkuu wa hifadhi ya Taifa ( TANAPA)  Dkt Alan Kijazi asema hali ya mto Ruaha mkuu ni mbaya kutokana na mto huo kwa sasa kuwa na maji kwa miezi minne pekee kwa mwaka.

Dkt Kijazi alimweleza makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo alipotembelea hifadhi ya Taifa Ruaha kuona uhifadhi wa ikolojia kwenye mto huo.

Alisema kuwa zaidi ya maji asilimia 56 yanayotumika kuzalisha umeme gridi ya Taifa kwa mabwawa ya mtera na Kidato hivyo pamoja na wanyama hifadhi hiyo ya Taifa ya Ruaha.

Hivyo alisema iwapo mto huo hautahifadhiwa na kuwepo kwa matumizi sahihi ya maji uhai wa mto huo na uhai wa wananya na wananchi zaidi ya milioni 6 wanaotegemea maji ya mto Ruaha.


Alisema kuwa matumizi yasiyo endelevu katika hifadhi ya ihefu mkoani Mbeya ni chanzo cha mto Ruaha kukauka.

Pia mgogoro wa hifadhi katika eneo la Chunya pia linachangia matumizi mabovu ya maji na kuwa shiriki limetumia bilioni 7 kutatua tatizo hilo japo bado tatizo lipo.

Mkurugenzi huyo alisema bilioni saba ni pesa nyingi sana ambazo zingetumika kwenye shughuli nyingine ila baadhi ya wanasiasa wanakwamisha zoezi hilo na kuchochea migogoro.

Aidha Dkt Kijazi alisema hali ya ujangili katika hifadhi hiyo inaendelea kutoweka japo bado kuna tatizo na jitihada zaidi zinahitajika kukabili ujangili.

Alisema ujagingili umepungua kwa asilimia 75 katika hifadhi hiyo ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Pia alisema kuwa TAMPA imejipanga kuongeza vitanda zaidi katika hifadhi hiyo ili kufikisha wageni wengi zaidi kutembelea na kulala kwenye hifadhi hiyo na kuwa tayari wameanza kutoa maeneo ya uwekezaji zaidi.

Dkt Kijazi alisema pamoja mipango mizuri ya kufungua lango la utalii hifadhi ya Ruaha ila ubovu wa miundo mbinu kutoka Iringa mjini hadi hifadhi ya Ruaha kumepelekea watalii wengi kutoka Afrika ya kusini waliokuwa wakitembelea hifadhi hiyo kwa sasa hawafiki kabisa.

Alisema mafanikio ya uhifadhi wa hifadhi hiyo yanatokana na ujirani mwema uliopo kati ya Shirika na jamii inayozunguka ambayo kwa sasa wanapatiwa miradi mbali mbali kwa lengo la kuinua uchumi wao.

Alisema jumla ya bilioni 3.5 zimekwisha tolewa na shirika kwa ajili ya kuchangia miradi ya kimaendeleo kupitia mradi wa ujirani mwema kwa mkoa wa Iringa ,Mbeya na Chamwino mkoa wa Dodoma.

Hivyo aliomba serikali kusaidia kunusuru bonde la usangu pamoja na kumaliza mgogoro wa usangu uliodumu kwa miaka 10 Sada.

Kwa upande wake makamu wa Rais Samia alisema kuwa serikali itahakikisha changamoto zote za mto Ruaha zinapatiwa ufumbuzi pia barabara kupiganiwa ili kuboreshwa zaidi.

Samia alitaka TANAPA kuendelea kushirikiana na wadau wa hifadhi kama MBOMIPA ambao ni wananchi wenye lengo la kulinda uhifadhi.

Hivyo alisema ni lazima wote kushirikiana kuhifadhi ikolojia ya bonde la usangu kwa uhifadhi wa mto Ruaha.

Huku waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi alisema kuhusu suala na migogoro ya ardhi ofisi yake ipo tayari kumaliza migogoro hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE