April 25, 2017

MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI 14.9 YAPITIWA NA MWENGE WA UHURU KILOLO, KIONGOZI WA MWENGE AONYA ISIBAGUE WANANCHI

Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa Asia Abdalah akitoa taarifa ya miradi ya mwenge itakayopitiwa na mwenge Kilolo baada ya kupokea mwenge toka wilaya ya Iringa 

idth="640" />
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Amour  Hamad Amour akisoma jiwe la msingi baada ya kuzindua ujezi wa ofisi ya kijiji cha kitelewasi leo,katikati ni mhamdisi wa ujenzi wilaya na kushoto mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour ametaka miradi nane yenye   thamani ya thamani ya shilingi bilioni 14.9 imezinduliwa na mbio za mwenye wa uhuru Kitaifa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa isiwabague wananchi. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo leo kiongozi huyo alisema baadhi ya wananchi wamekuwa na mitazamo tofauti juu Mwenge wa uhuru wakipotosha kuwa mwenge huo ni wa CCM hivyo miradi hiyo inawahusu wana CCM jambo ambalo si kweli kwani miradi na mwenge huo ni haki ya watanzania wote. 

Hivyo alitaka miradi hiyo kutunzwa na kuwanufaisha wananchi wa vyama vyote na wasio na vyama na kuwa ni wajibu wa viongozi wa vyama vyote kushiriki katika mbio za mwenge. 

"Miradi hii ni miradi mizuri na ni miradi ya watanzania wote na hakuna chama chenye hati miliki na mwenge hivyo wote tushiriki kuupokea mwenge na kutumia miradi hii na kila mmoja kutunza miradi hii"

Kiongozi huyo alisema mwenge wa uhuru huleta umoja, upendo na mshikamano kuwa katika kuendeleza hayo ni vema kila mtanzania kuenzi mbio za mwenge wa uhuru. 

Amour alisema kuwa mwenge wa uhuru ni mali ya watanzania wote hivyo jukumu la kuchangia miradi ya kimaendeleo ni jukumu la watanzania wote bila kubaguana kiitikadi.

Aidha alisema kuwa moja kati ya sera ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya uchumi wa viwanda hivyo ni jukumu la kila mtanzania kujipanga kunufaika na viwanda hivyo pia kuzalisha zaidi. 

Pia ataka wakandarasi wanaojenga miradi kujenga kwa kiwango kinacholingana na pesa walizolipwa badala ya kujenga kiubabaishaji. 

Kuhusu Vita ya dawa za kulevya inayoendelea nchini alitaka wananchi kumuunga mkono Rais Dkt  Magufuli kwani ana nia ya dhati kuona Tanzania inakuwa na vijana wasio athirika na dawa za kulevya.

Akisoma taarifa ya utii kwa Rais mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa wilaya hiyo imeendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo kwa faida ya wananchi na kuwa wananchi wamekuwa mstari wa mbele kuchangia miradi hiyo Katika miradi hiyo nane iliyopitiwa na mwenge mwaka huu wananchi wamechangia kiasi cha shilingi milioni 4.7

Wakati halmashauri imechangia zaidi ya shilingi milioni 25,wadau wa maendeleo wamechangia 880,000 ,madiwani wa halmashauri ya Kilolo wamechangia 710,000 huku watumishi wamechangia milioni 5.6 na taasisi zimechangia 700,000.

Alitaja miradi hiyo nane iliyopitiwa na mwenge kuwa ni miradi ya ofisi ya kijiji, elimu, barabara, afya, viwanda, skimu ya umwagiliaji, miradi ya uvuvi ya vijana pamoja na klabu ya wanafunzi ya wapinga rushwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE