April 3, 2017

MEYA HALMASHAURI YA DODOMA ATUMBULIWABaraza la Madiwani Manispaa ya Dodoma limemvua uongozi mstahiki  meya wao Jafari Mwanyemba kwa tuhuma za kutafuna shilingi milioni 30 za mradi wa maji katika kijiji cha Zuzu kilichopo Manispaa ya Dodoma,fedha zilizotolewa na Serikali ya Japan mwandishi wa matukiodaimablog Dodoma Upendo John anaripoti.

Kuwa hatua hiyo ya madiwani hao ambao  56  walihudhuria kikao hicho walifikia uamuzi wa kupiga kura na kura  47 zilimkataa hivyo kupoteza nafasi hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi aliratibu zoezi la upigaji kura  wakati  Mbunge wa Jimbo hilo Antony Mavunde na Mkuu wa Wilaya hiyo,Christina Mndeme walipata kushiriki kikao hicho.

Madiwani hao mara kwa mara walikuwa wakimtuhumu meya huyo kwa tuhuma za ufisadi kabla ya leo kupiga kura za kutokuwa na imani naye.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE