April 24, 2017

MESSI ALIVYOIUA REAL MADRID JANA USIKU


Lioneil Messi “La Pulga” alikuwa na usiku mzuri sana baada ya kuwa mstari wa mbele kuiangamiza Real Madrid katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.
Real Madrid ndio walitangulia kuliona lango la Barcelona katika dakika ya 28 tu ya mchezo kupitia kwa Casemiro kabla ya Lioneil Messi kuwasawazishia Barcelona na kwenda mapumziko kwa sare ya moja kwa moja.
Kipindi cha pili Barcelona walipata bao la pili lililofungwa na Ivan Ractic na wakati Madrid wakiwa katika juhudi za kusawazisha walipata tatizo baada ya nahodha wao Sergio Ramos kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Kadi nyekundu haikuwadhuia Real Madrid kuwaandama Barcelona na katika dakika ya 86 James Rodriguez aliyeingia akitokea benchi aliipatia Real Madrid bao la kusawazisha.
Hadi inafika dakika ya 90 matokeo yalikuwa ni mbili kwa mbili, mashabiki wakiamini mchezo unaisha kwa sare Lioneil Messi tena dakika za nyongeza alikokota mpira na kuifungia Barcelona bao la tatu.
Messi ambaye amekuwa kinara wa El Classico mara nyingi hilo lilikuwa goli lake la 500 kwa timu yake ya Barcelona, na matokeo hayo yamewafanya Barcelona kuwa alama sawa na Madrid huku Madrid wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE