April 5, 2017

MATOKEO YA UCHAGUZI UBUNGE EALA CCM WASHINDA, CHADEMA WAGOMBEA WAO WAKATALIWA .


Taarifa za awali kutoka Bungeni zinadai kuwa wagombea wa CCM mambo safi bunge la Afrika mashariki baada wagombea wao 6 kushinda huku wagombea waupinzani wakishindwa baada ya wabunge kukosa imani nao 

Hawa ndio wa CCM walioshinda ni pamoja na 
1. Fancy Nkuhi (ke)
2. Happiness Legiko (ke)
3. Maryam Ussi Yahya (ke)
4. Dkt Abdullah Makame (me)
5. Dkt Ngwaru Maghembe (me)
6. Alhaj Adam Kimbisa (me).

Nafasi za Upinzani:
Wagombea wawili wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje wamepigiwa kura nyingi za HAPANA hivyo hawajachaguliwa kuwa wabunge. 

Masha na Wenje kwa pamoja wamepigiwa kura 126 za NDIYO, na kura 198 za HAPANA. 

Kufuatia matokeo hayo nafasi 2 za Chadema kwa EALA zitaendelea kuwa wazi, na Chadema itahitaji kupeleka wagombea wengine bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura.!


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE