April 18, 2017

MASHINDANO YA VILLA CUP 2017 YAANZA KUTIMUA VUMBI MUFINDI

mratibu wa mashindano ya Villa Cup kulia akiteta jambo na mgeni rasmi
Mratibu wa mashindano ya Villa Cup akiwa na wachezaji pamoja na mgeni rasmi 
Mgeni rasmi akitoa hotuba yake ya ufunguzi 
MKUU wa wilaya ya Mufindi Jamhuri wiliam azindua mashindano ya Villa Cup 2017 ambayo yameshirikisha timu 36 za wilani Mufindi mkoa wa Iringa kwa lengo la kuunga mkono serikali katika sekta ya michezo .

Mratibu wa mashindano hayo Dickson Villa alisema kuwa mashindano hayo yameanza toka mwaka 2013 na kuwa pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali kupitia wizara ya michezo ,utamaduni na sanaa bado mashindano hayo yatasaidia kuinua vipaji vya vijana na kuongeza ajira kwa wachezaji hao kupitia michezo.

Alisema kuwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo ni kampuni yake ya Villa Express na kuwa mashindano hayo ni sehemu ya ahsante kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi ambao wamekuwa wakitegemea kampuni yake kwa usafiri wa ndani ya wilaya na nje ya wilaya hiyo.

Villa alisema kuwa mashindano hayo yataendelea kwa miaka yote na kuomba wadhamini zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo yenye kauli mbiu ya Mufindi bila madawa ya kulevya inawezekana.

Pia aliwataka vijana kuachana na kushinda vijiweni na badala yake kujihusisha na michezo ama shughuli za kuwaingizia kipato na kuwa suala la michezo ni moja ya tiba kwa magonjwa yasiyoambukizwa kama ambavyo serikali kupitia makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan imeagiza kila mwananchi kufanya mazoezi kila wiki kwa afya yake .

Akizungumzia zawadi kwa bingwa wa mashindano hayo kuwa bingwa atapata shilingi 800,000 na kombe lenye thamani ya shilingi 200,000 wakati mshindi wa pili atapewa ng'ombe mnyama huku mshindi wa tatu atapewa shilingi 100,000
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mufindi diwani wa kata ya Makungu Kizito Kambo alisema kuwa vijana wa Mufindi wataweza kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na hata kuweza kujipatia ajira katika timu mbali mbali ikiwemo ya Lipuli Fc ambayo imepanda daraja na msimu ujao kucheza ligi kuu Tanzania bara .

Alisema kuwa tatizo la dawa la kulevya kwa vijana limeendelea kuota mizizi na mkuu wa wilaya ya Mufindi amekuwa mstari wa mbele kupiga vita matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya katika wilaya hiyo hivyo kupitia michezo hiyo ni matumaini yake vijana wengi watajikita katika michezo badala ya kujihusisha na dawa za kulevya.

Hivyo aliwataka vijana wanaoshiriki mashindano hayo kucheza kwa kuzingatia nidhamu na kuepuka vurugu wakati wote wa mashindano hayo kwani wengi wao wanafuatilia na pale watakapocheza kwa nidhamu ni rahisi zaidi kuchukuliwa na timu mbali mbali .

Alisema wilaya ya Mufindi ni moja kati ya wilaya ambazo zina wachezaji wazuri ambao wamepata kushiriki mashindano ya kombe la Muungano Mufindi na sasa kombe la Villa ambalo limeanza kurejesha wilaya ya Mufindi katika uhai wa soka .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE