April 17, 2017

MANISPAA YA IRINGA YAPUUZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS? RC IRINGA TUMBUA JIPU

Hivi ndivyo  wananchi  Iringa  mjini  walivyovamia  mlima  Ipogolo na  kufyeka miti kwa  ajili ya ujenzi wa vibanda  vya biashara 
Wananchi  Manispaa ya  Iringa  wavamia  Mlima Ipogolo  wajipimia  viwanja  vya kujenga vibanda  vya  biashara 
Wananchi  mjini Iringa  wakiendelea  kufyeka  miti  kuandaa maeneo ya  biashara
Soko la Magari  mabovu  Kitanzini  ambalo  watahamia wafanyabiashara  wa Mashine tatu


ZIKIWA  nimepita  takribani  siku nne  toka  Makamu  wa  Rais  wa Jamhuri ya  muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan  kuzindua kikosi kazi  cha uhifadhi  wa Ikolojia  mto  Ruaha  mkuu  na  kuagiza mkoa  wa Iringa  kulinda  milima pamoja na kutunza mazingira , Idara ya  Mazingira  na  Misitu  katika  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  imepuuza agizo hilo baada ya kuacha  wananchi  kuvamia  mlima Ipogolo  kwa  ujenzi wa vibanda  vya biashara .

Mtandao  wa  matukiodaimaBlog  umetembelea eneo hilo na kushuhudia  wananchi  wakiendelea  kufyeka miti ya  asili  na  kuvunja  mlima  huo uliohifadhiwa na  kujenga  vibanda  vya biashara  huku  ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo  ikitazama pasipo  kuchukua hatua  zozote .

Uharibifu  mkubwa  unaofanywa katika  mlima huo  ukifumbiwa macho kama  ilivyo  ni   wazi  uongozi wa Manispaa ya  Iringa  umepuuza agizo  hilo la makamu wa Rais  na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto  Ruaha kwa  mwendo huo itakuwa ni  ndoto  ya alinacha .

Hii ni aibu  kwa  viongozi wa Halmashauri  hii kuacha  uharibifu  huu wa mazingira  kufanywa  eneo la mboni za macho yao  na  kama uongozi wa  mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza usipo  chukua hatua kwa idara ya mazingira na misitu  ni sawa na kuruhusu wananchi  hao  kuendelea na uvamizi hii .

Kuna  hatua  za  wazi ambazo Manispaa ya  Iringa inapongezwa  ikiwemo ya  kuanza kuwaandalia  soko wafanyabiashara   hao wa Mashine tatu  ambao  eneo  walilokuwepo  la Mashine  Tatu kuhitajika na Bakwata  ambao  waliazima  kwa  muda na  sasa  muda wao umekwisha .

Ila  pia uamuzi wa  kuwaleta  wafanyabiashara  hao soko la Mashine Tatu ni  mzuri  kwa  kunusuru  soko  hilo  lililojengwa kwa  mamilioni ya shilingi  ila  lilikuwa  halitumiki ipasavyo .

Lakini kwa uharibifu  huu  wa Mazingira  sitanyamaza   na kubaki  kusifia uvujifu  huu wa  sheria za mipango  miji na sheria za Mazingira na misitu  kwani  kuruhusu  uvamizi huu wa mlima Ipogolo ni utovu  mkubwa wa nidhamu kwa makamu wa Rais  aliyeagiza  mazingira  kutunzwa.

Hivi kwa  upuuziaji  huu wa sheria  ikolojia  ya  mto  Ruaha  itahifadhiwa kweli ama ndio kusema  maagizo ya makamu wa Rais kwa Manispaa ya  Iringa ni sawa na kumpigia  gitaa mbuzi ?


Uko  wapi mkuu  wa  wilaya ya  Iringa kakangu  Richard Kasesela  maana  Manispaa wameshindwa kumheshimu makamu  wa Rais kwa  kuruhusu mazingira  kuharibiwa  yawezekana  ukisema  wewe ama kwenda  kutembelea  eneo  hilo utajua kama  huu ndio  uhifadhi wa mazingira alioutaka makamu  wa Rais ?

Naomba mkuu  wa mkoa wa Iringa mama  Amina Masenza katika  hilo tumbua jibu  hilo  Manispaa ya  Iringa  kwani  haiwezekani mazingira  yakaharibiwa   hivi mtu  wa mazingira  yupo ,afisa  misitu  yupo na sina hakika kama mkurugenzi wa Halmashauri hajaliona  hili na kama hajaona  hivi ndio  kusema Kitanzini haina afisa mtendaji wa kata ama mtaa vipi wanyamaze  Kimya ? nimesema  sitanyamaza  kimya kwa  hili.

USIKOSE  MWENDELEZO  WA SAFARI  HII HAPA HAPA  MATUKIODAIMA


  

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE