April 2, 2017

MALI YA MTOTO WA KIKE WA RAIS TRUMP NA MUMEWE YATISHA

Ikulu ya Marekani, imetoa maelezo kuhusu mali ya binafsi ya watu waliomo katika serikali ya Rais Donald Trump.

Mali hiyo imedhihirishwa kama sheria inavyoelekeza, na inaonyesha kuwa mtoto wa rais wa kike, Ivanka pamoja na mumewe Jared Kushner, wana takriban dola milioni 240 na 740 mtawalia.

Hii ni pamoja na hisa kwenye hoteli ya Trump International, ambazo zilimpa Ivanka kati ya dola milioni 1 na milioni 5 mwaka uliopita.

Ufichuzi huo wa mali pia unaonyesha mishahara na watu wengine wa vyeo vya juu uongozini.

Nyaraka zilizotolewa pia zilionyesha mali wakati wakianza kuifanyika kazi serikali na kabla la mali yoyote kuuzwa

    Ivanka Trump kupewa ofisi White House

    Wanawake 20 matajiri zaidi duniani 2017
    Vijana 10 matajiri zaidi duniani
    Watu wanane matajiri kupindukia duniani

Ikulu ya White House inajaribu kuonyesha kuwa watu katika serikali ya Trump wanajiweza, na inasema watu hao wamejitolea sana kwa kukubali kutumika serikalini.

Watu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.#Chanzo BBC#

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE