April 28, 2017

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI SIKU YA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU LEO

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suhulu Hassan leo ijumaa  anatarajiwa kuwa mgeni rasmini katika siku ya watetezi wa haki za binadamu jijini Dar es Salama. 

Mratibu wa mtandao   wa  watetezi  wa  haki  za  binadamu (THRDC) Onesmo Ole Ngurumo amesema maadhimisho hayo yatafanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl kuanzia kuanzia asubuhi. 

Alisema kila mwaka mtandao wa THRDC umekuwa ukifanya maadhimisho hayo kwa na kabla ya maadhimisho hayo hutanguliwa na mafunzo mbali mbali kwa wanachama wake .

 asasi  za  kiraia hazipo kwa kazi ya  uchochezi   wala  kugombana na  serikali kama  ambavyo  baadhi ya  viongozi  wa serikali  wanavyozitazama asasi hizo .

kuwa kila mwaka wamekuwa wakialika viongozi wa mbali mbali wakiwemo wa serikali ili kuweza kujua shughuli zinazofanywa na asas za kiraia .

Alisema Kuwa asas hizo zipo  kwa  mujibu wa  sheria  na  zinafanya kazi  yake kwa  kuzingatia sheria  hivyo kuendelea kuwa na mtazamo  tofauti kwa kuziona ni adui.  


Alisema  kuwa  kuna  baadhi ya  maofisa wa  serikali  wanashindwa  kuzielewa  vizuri  asasi  za  kiraia na  kuona kama  ni  wachechezi ama watu  wanaoigombanisha  serikali  na  wananchi  japo  ukweli  kazi kubwa imekuwa  ikifanywa na asasi  hizo  kwa  ajili ya  kuisaidia  serikali .

“ Kwa mujibu  wa  sheria  asasi  za  kiraia  zipo  kwa  ajili ya kuangalia  wapi  pamekosewa  na  kutoa  ushauri  na  kukosoa ila  pia asasi  hizi  zipo  kwa  ajili ya  kusaidia  pale  ambapo serikali  imeshindwa  kusaidia  ndio maana  zipo  asasi  zinazojenga  shule ,zahanati na shughuli nyingine za  kijamii “

Hata  hivyo  alisema  njia  pekee  ya  kuwafikia  wananchi ni pamoja na  kuwaacha  wananchi hao  kutoa maoni  yao  na  sio  kuwanyima  uhuru  wa  kutoa maoni na kuwa  nchi  zilizo nyingi  za  kiafrika zinawanyima  watu  wake  uhuru wa  kutoa maoni yao .

“ Sehemu  kubwa  kwa nchi  ambayo inazuia uhuru wa  watu  wake  kutoa maoni yao  huwa  haipendi  kuona  asasi za  Kiraia  zikisema hivyo  ndio  sababu ya  kuziona  asasi  hizo  kama adui  jambo  ambalo  asingependa asasi  za  kiraia  nchini  kutazamwa kama adui wa  serikali “

Mratibu  huyo  alizitaka  asasi  za  kiraia  kuendelea  kufanya kazi yake  bila  kuogopa  kwani  wapo  kwa  ajili ya  kuwatumikia  wananchi na  kushirikiana na  serikali  kuibua  changamoto  zinazoikabili jamii na kuzifanyia kazi kwa  zile  zinazowezekana kufanywa na asasi  hizo.

Kuhusu suala la waandishi wa habari nchini  kuendelea  kupigwa kama  ilivyotokea katika   kikao  cha  chama  cha  wananchi (CUF) alisema  wanaendelea  kuorodhesha matukio  hayo na  watatoa  ripoti  japo  kwa  sasa  mtandao  wa THRDC  unalaani  vitendo   hivyo na  kutaka  wanahabari  nchini  kutonyanyaswa .

Alisema  wanaendelea  kufuatilia  matukio  yote ya  wanahabari  kunyanyaswa  kwani  wapo  ambao  wamenyanyaswa na   viongozi  wa  serikali na  wapo  walionyanyasika  na wafuasi wa  vyama  vya  siasa na  kuwa  ripoti yao  wataitoa  siku  maadhimisho  ya uhuru  wa  vyombo  vya habari

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE