April 9, 2017

MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA SIKU NNE IRINGA

Na MatukiodaimaBlog

MAKAMU wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania samia Suluhu Hassan kufanya ziara kesho (Jumatatu) mkoani Iringa. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo  ofisini kuhusu ziara hiyo mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa lengo la ziara hiyo ya siku nne mkoani Iringa ni kuhakiki mfumo wa ikologia kwenye mto Ruaha Inayohifadhiwa na mto kuwa endelevu. 

"mheshimiwa makamu wa Rais atawasili kesho tarehe 10 jioni na atakuwepo mkoani hapa hadi tarehe 13 "

Alisema Siku inayofuata ya tarehe 11 makamu wa Rais ataongoza kikao cha uhifadhi endelevu wa mfumo wa ikologia mto Ruaha mkuu. 

Wakati tarehe12 ya mwezi huu mama Suluhu  atatembelea mto Ruaha kuona uhalisia kabla ya kuondoka Tarehe 13 majira ya saa 3 asubuhi. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kulinda vyanzo vya maji vyote katika mto huo Ruaha na kuwataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vyote vya maji. 

Hii ni ziara ya kwanza kwa makamu wa Rais kufanya ziara yake mkoani Iringa toka serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuingia madarakani. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE