April 11, 2017

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKUTANO WA KWANZA WA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA BONDE LA MTO RUAHA MKUU

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa taarifa ya mkoa mbele ya makamu wa rais leo

Wadau wa mkutano wa kikosi kazi cha kunusuru mto Ruaha mkuu wamekutana katika mkutano wa kwanza wa kikosi kazi cha kitaifa mkoani Iringa chini ya makamu wa Rais Samia suluhu. 

Katika kikao hicho kinachoendelea ukumbi wa siasa ni kilimo mjini Iringa kikao  ambacho kimeshirikisha mawaziri mawatu akiwemo wa Ardhi, Mazingira na maliasili ,waziri wa mazingira January  Makamba ametambulisha kikosi kazi chake. 

Mto Ruaha mkuu umekuwa ni mto tegemeo kwa watu zaidi ya milioni 6 ambao wanategemea mto huo ambao kwa sasa serikali imekuja na mkakati kabambe wa kulinda mto huo. 

Hatua ya serikali kupanua pori la akiba ya usangu kuingia katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha kumeendelea kulinda maji ya mto Ruaha mkuu. 
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE