April 10, 2017

MAKAMU WA RAIS APONGEZA MKOA WA IRINGA

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu amesema atapanga ziara rasmi mkoa wa Iringa ila kwa sasa amekuja kunusuru mto Ruaha mkuu usitoweke. 

Akitoa salamu zake leo baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Iringa alisema kuwa mto Ruaha unasikitisha. 

Huku akitaka wadau wote na viongozi wa mkoa kusimamia mto huo usitoweke. 

Katika hatua nyingine makamu wa Rais amepingana na tafiti ya kuwa watanzania tunaishi chini ya dola moja na kuwa watanzania tuna uwezo wa kula matunda zaidi ya matatu na kuwa tunaishi kitajiri zaidi japo umasikini wetu ni wa kujitakia. 

Alisema kuwa ni vema viongozi kusimamia vizuri fedha za TASAF ambazo ni fedha ambazo zitakuja lipwa na vizazi vijavyo. 


Hivyo alitaka walengwa wa pesa za TASAF wawe ni wale ambao wamelengwa isiwe kama mkoa wa Arusha ambao wametoa fedha hizo kwa watu ambao si walengwa. 

Kuhusu ufaulu mzuri wa elimu na afya ya mama na mtoto alisema mkoa wa Iringa umefanya vizuri sana kitaifa. 

Japo alisema mkoa huo unatia aibu katika maeneo mawili ya Ukimwi na lishe kuwa mkoa wa Iringa ni aibu kuwa na udumavu kwa watoto.

Wakati huo huo makamu wa Rais amepongeza kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa kwa kazi nzuri ya kuufanya mkoa huo kuwa salama. 

Huku akiwataka wananchi kutoa taarifa mapema za kuwatumbua wale wote wanahisiwa ni waarifu. 

Alisema Tanzaniani ni nchi inayovutia hivyo wapo wanaotumika kuvuruka nchi hii. 
awali serikali ya  mkoa wa Iringa katika taarifa yake kwa makamu wa Rais ilisema kuwa hali ya kisiasa ndani ya mkoa wa Iringa imetulia na hakuna vurugu zozote zinazoendelea. 

Akitoa taarifa hiyo mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema pamoja na hali ya kisiasa kuwa shwari Ndani ya mkoa bado hali ya ulinzi na usalama mkoa ni shwari. 

Hata hivyo alisema kwa upande wa hali ya chakula mkoa unataraji kupata zaidi kwa kuwa na uhakika wa kuvuna zaidi huku tani 84,000 zinategemewa kuvunwa kwa mazao ya biashara. 

Huku tani 11000 za mbolea mkoa huo jumla ya hekari zaidi ya 200000 kwa ajili ya malisho kwa wafugaji. 

Makamu wa Rais Leo ataendesha kikao cha uhifadhi wa Kibailogia katika mto Ruaha mkuu kikao kitakachofanyika ukumbi wa siasa ni kilimo mjini Iringa na kesho atatembelea mto Ruaha wakati kesho kutwa asubuhi ataondoka mkoani Iringa. 0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE