April 17, 2017

MAJI YA MVUA YA MTO RUAHA MKUU HAYAJAFIKA BWAWA LA MTERA

Waziri wa Mazingira na muungano January Makamba akitazama mto Ruaha mkuu eneo la hifadhi ya Taifa Ruaha
.........................................
Na MatukiodaimaBlog 

PAMOJA na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Iringa mwaka huu imeelezwa kuwa maji ya mto Ruaha mkuu hadi sasa bado hayajafika bwawa la Mtera linalozalisha umeme Gridi ya Taifa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira na matumizi yasiyosahihi ya maji ya mto huo.

Meneja wa kituo hicho mhandisi John Sikauki alisemweleza makamu huyo wa Rais Samina Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani Iringa kuwa pamoja na kuwa hali ya maji katika Bwawa la Mtera si mbaya na kuna uwezekano wa maji hayo kuendelea kuzalisha umeme hadi Octoba mwaka huu japo hadi sasa maji waliyopo kwenye bwawa hilo ni kutoka katika mito mito midogo na mto Kisigo ila mto Ruaha mkuu ambao tegemeo kubwa hadi sasa maji yake hayajafika katika bwawa hilo .

Alisema hali ya maji na ufuaji wa wa umeme katika kituo hicho kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha mwaka 2015 kina cha juu cha maji katika bwawa la Mtera kilifikia mita 690.94 tu juu ya usawa wa bahari na kuwa kina kiliendelea kushuka kutokana na uzalishaji hadi Octoba 7 mwaka 2015 kilifikia mita 687.54 juu ya usawa wa bahari hali iliyofanya kituo kusitisha ufuaji umeme
Hata hivyo alisema kina kiliendelea kupanda mwanzoni mwa Januari 2016 kuanzia mita 668.26 juu ya usawa wa bahari na mbaka Januari 23 mwaka 2016 kina kilifikia mita 689.68 juu ya usawa wa bahari ndipo ufuaji umeme ulianza .

Kuwa kina cha maji hadi kufikia mwezi Aprili 2017 ni mita 693.76 ju ya usawa wa bahari na kuwa kina hicho kina uwezo wa kuzalisha umeme hadi mwishoni mwa mwezi Oktoba bila maji yam to Ruaha mkuu kuingia na iwapo maji ya mto Ruaha mkuu ambayo bado kufika Bwawa la Mtera yataingia basi kuna uhakika wa uzalishaji kuendelea zaidi.

Aidha alisema hali ya mitambo ya uzalishaji wa umeme ipo vizuri kwa sasa ambapo kwa sasa mpango wa matengenezo kwa kuzingatia umri wa mitambo wa mwaka28 umekwisha anza wakati matengenezo makubwa yalikwisha fanyika ikiwa ni Pamoja na ukarabati wa wa Genereta zote mbili.

Kwa upande wake makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza wakuu wa mikoa ya Njombe , Mbeya na Iringa kuhakikisha wanalinda bonde la Usangu kwa kutazama shughuli zinazohatarisha mto Ruaha mkuu kukauaka .

Kuwa serikali haikatazi wananchi kufanya shughuli za kiuchumi ila wanataka kuona shughuli zinazofanyika zinazingatia sheria za matumizi bora ya maji .

“ Wananchi wafanye shughuli za kiuchumi lakini bado wasiikatishe ile ikolojia ambayo ipo ambayo mwenyezi Mungu aliiweka kwa manufaa yetu sote …. shughuli za binadamu zinazochepusha maji basi zitazamwe kwa mwelekeo wake “

Hata hivyo Makamu huyo wa Rais amesifu kazi inayofanyika katika kituo cha ufuaji wa umeme Mtera Pamoja na usimamizi mzuri wa bwawa la Mtera ambalo kwa sasa limesimamiwa vizuri na kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa uhakika hadi Octoba mwaka huu .

“Taarifa za kusikia na kusoma katika vyombo mbali mbali vya habaari ili kuwa ni vigumu kujua kazi inayofanyika katika bwawa la mtera ila baada ya kufika nimejifunza na kuona kazi nzuri inayofanyika hapo”

“ Kweli mnajituma kutunza hiki kituo na kuhakikisha kuwa taifa halipati adha ya kukatika umeme nimeona na nawapongeza sana kwa kutunza bwawa la mtera na kuendesha kituo hiki”

Alisema kuwa lengo la kufika mkoani Iringa ni kuzindua kikosi kasi cha kufufua na uhifadhi wa ikolojia katika mto Ruaha kuu kupitia bonde la Usangu linalomwaga maji yake Ruaha mkuu kukata mawasiliano kabisa na Bwawa la Mtera .

Alisema kuwa kuna tatizo kubwa kubwa la matumizi ya maji katika mto Ruaha mkuu na hivyo serikali imelazimika kuunda kikosi kazi kitakachohusisha wizara zote kwa ajili ya kunusuru mto huo wa ruaha mkuu ambao unategemewa na watu zaidi ya milioni 6 kama si milioni 8 .

Hivyo alisema kikosi kazi hicho kitawezesha wataalam kukaa chini na kusoma Ikolojia kutoka Ihefu ili kuona ni kwa njia zipi zitumike kwa ajili ya kunusuru mto huo pia wanyama na wananchi wanaotegemea mto huo kuendesha maisha yao .

“ Baada ya wataalam hao kukaa na kuandaa ripoti yao serikali itaifanyia kazi ripoti hiyo na kuja na nini cha kufanya kwa serikali kuchukua hatua kwa nafasi yake pia jamii nayo kuchukua hatua kwa upande wake ili kuufanya mto huo kurejea katika viwango vyake vya kutiririsha maji mwaka mzima”

Alisema kuwa kuna haja ya Taifa kutoa kipaumbele cha pekee katika bonde hilo kuona linatiririsha maji muda wote japo suala hilo halitafanywa kwa haraka ila litafanyika kwa hatua kwa hatua ili kuona ufumbuzi wa kweli unafanyika .

 Wakati huo huo shirika la hifadhi ya Taifa ( TANAPA) limedai kumia kiasi cha Shilingi bilioni saba kulipa fidia na gharama nyingine kunusuru bonde la usangu kwa ajili ya mto Ruaha mkuu bila mafanikio.

mkurugenzi mkuu wa TANAPA Dkt Allan Kijazi alisema kuwa mbali ya shirika kutumia kiasi hicho kikubwa cha pesa kulipa fidia kwa ajili ya kunusuru mto Ruaha mkuu lakini bado zipo changamoto zinazoathiri usimamizi wa eneo na zinahitajika uamuzi wa serikali.

Dkt Kijazi alisema shirika lake linapongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Jonh Magufuli kwa kuomyesha ushirikiano mkubwa wa kusimamia hifadhi ya mazingira na Raslimali kwa ujumla.

"Tunaimani kuwa kwa jitihada hizi tunaweza kuboresha mazingira na viumbe kwa manufaa mapana ya kizazi cha sasa na kijacho "

Hivyo alisema ombi la shirika kwa makamu wa Rais na serikali kwa ujumla kuzidi kusaidia katika kunusuru bonde la usangu ili liweze kurejesha mtiririko wa maji kwa ajili ya matumizi ya hifadhi ya Ruaha, mabwawa ya Mtera na kidato na pia kwa ajili ya matumizi ya wananchi wengine walio katika maeneo ya chini ya mkondo wa maji ya mto Ruaha.

Kuwa mikakati ya uhifadhi wa mto Ruaha iende sambamba na kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi na wananchi ambao umedumu kwa miaka takribani kumi sasa toka mwaka 2008 mkoni Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE