April 4, 2017

MADIWANI MKOA WA IRINGA WASEMA WALIKUWA WANAFANYA KAZI HIYO BILA WELEDI , RC MASENZA AWATAKA KWENDA KUTUMIKIA WANANCHI KIWELEDI ZAIDI ......

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  akiwa  katika  picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya   ya wilaya ya  Mufindi pamoja na madiwani na mkuu wa wilaya ya  Mufindi  Wiliam Jamhuri wa pili  kulia  waliokaa
Mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  akifungua  warsha  ya  siku mbili ya madiwani wa Halmashauri za  mkoa wa Iringa
Baadhi ya  madiwani wa Halmashauri   tatu za mkoa  wa Iringa wakiwa katika  warsha ya  siku  mbili ya  kuwajengea  uwezo leo mjini Iringa  wa kwanza  kushoto ni mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  Alex Kimbe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi Festo Mgina
Madiwani  wakiwa katika  warsha hiyo  leo
Das  Iringa  akifuatilia  mafunzo hayo
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika  picha ya pamoja na madiwani wa Manispaa ya  Iringa
Mkuu  wa mkoa wa Iringa katika  picha ya pamoja na madiwani wa mji  Mafinga
 Na MatukiodaimaBlog
MADIWANI mkoani Iringa wadai kutokana na  kutokuwepo kwa mafunzo  mbali mbali toka  walipochaguliwa mwaka 2015 walikuwa  wakiwatumikia kwa kutumia vipaji vyao na kupelekea baadhi ya Halmashauri kuingia katika kashfa za matumizi mabaya  ya  fedha.

Wakizungumza  leo  baadhi ya madiwani  katika  mafunzo ya  kuwajengea  uwezo  yaliyofanyika mjini Iringa kwa Halmashauri tatu  za mkoa wa Iringa , madiwani hao  walisema kwa  muda  sasa  wamekuwa  wakishiriki  kwenye vikao  vya maamuzi bila kujua majukumu yao .

Akizungumza  kwa niaba ya  madiwani  wenzake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya  Mufindi  Festo Mgina  alisema  kuwa  mafunzo hayo  ya  uongozi ambayo  yameanza  kutolewa  leo na kesho   yatawajengea  uwezo madiwani hao  kuweza  kufanya maamuzi mbali mbali kwa  weledi zaidi  tofauti na  mwanzo .

“ Mafunzo hayo  tulipaswa  kupewa kabla ya  kuanza  kazi ya  kuwatumikia  wananchi  ila hayakuweza  kutolewa   hivyo  wengi  wetu  tulikuwa tukitumia  uzoezi   binafsi ama kwa  wale  waliotangulia ila matokeo yake  ni  kufanya  vizuri na vibaya kulikuwa ni moja ya  matokeo ya kufanya kazi bila mafunzo”

Joseph Lyata  ni naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa alisema  kuwa mbali ya mazuri ya  waliotanguliwa  ama madiwani  wazoezi  kutumika kujifunza ila baadhi ya maamuzi mengi hayakuwa mazuri na   hivyo matokeo yake miradi mingi iliyofanywa na watangulizi  baadhi ya miradi  kuwa  chini ya  kiwango .
Hivyo  alisema kuanzia  sasa  baada ya mafunzo hayo  wataweza  kuwatumikia  vema wananchi  wao  na kutumia baraza la madiwani  kuwawakilisha  wananchi badala ya kuvutana  kisiasa .

Akifungua mafuzo hayo  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya Rais Dkt  John Magufuli inatambua mchango mkubwa  unaofanywa na wadau mbali mbali wa maendeleo na nchi wahisani wakiwemo watu wa Marekani ambao wanafadhili Mradi huu  wa kuwapatia uwezo madiwani pamoja na mafunzo haya  kupitia Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID). 

Alisema  kuwa msaada wao kwa Mkoa  wa Iringa ni mkubwa, kwani PS3 ni mradi wa kipekee kwa maana ya kugusa eneo la mifumo ambalo ni eneo mtambuka kwa sekta zote, kinyume na mazoea ya kuwa na miradi ambayo inalenga sekta moja moja.
 
 “Hii ina maana PS3 wako makini katika kuendesha shughuli zao kwa kufuata taratibu ambazo tunakubaliana nao. Atimizaye ahadi ni muungwana….Mafunzo haya kwa Madiwani wa Manispaa ya Iringa, Halmashauri ya Mji wa Mafinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi yana umuhimu wa kipekee sana. ..ni mafunzo yanayolenga kumwongezea ujuzi “

Alisema kwa  lengo la kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani linatokana na sababu kama madiwani waliochaguliwa ama kuteuliwa, wanatokana na taaluma na fani tofauti-tofauti, hivyo upo umuhimu wa kuwajengea uwezo, kuwapa maarifa na mtazamo wa pamoja juu ya usimamizi na uendeshaji wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Muundo wa Serikali za Mitaa, Sheria za Serikali za Mitaa, na masuala mtambuka katika jamii, ikiwemo masuala ya Ukimwi, Jinsia, na Makundi Maalum ni  vema wakitoka kwenda  kutumia mafunzo hayo kubadili halmashauri  zao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE