April 11, 2017

KOREA KASKAZINI YASEMA ITATUMIA SILAHA KALI ZA KIVITA DHIDI YA MAJESHI YA MAREKANI

 Wanamaji wa Marekani waliotumwa katika eneo la magharibi mwa bahari ya Pacific

Korea Kaskazini imesema kuwa itajitetea kwa kutumia silaha kali ili kujibu hatua ya Marekani kupeleka wanamaji wake katika rasi ya Korea.

Wizara ya maswala ya kigeni ilinukuu shirika la habari la serikali KCNA lililosema kuwa hatua hiyo ya Marekani inaonyesha uvamizi wa kijinga uliofika awamu yenye hatari kubwa.

Jeshi la Marekani katika maeneo ya Pacific limesema kuwa hatua hiyo inalenga kuonyesha Marekani imejiandaa kwa lolote lile.

    Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
    Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
    Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa

Rais Trump amesema kuwa Marekani imejiandaa kibinafsi kukabiliana na tishio la nyuklia linaloletwa na Korea Kaskazini.

Wakati huohuo Korea Kusini na China ambaye ni mwandani wa Korea Kaskazini wameonya kuchukua hatua kali dhidi ya Pyongyang iwapo itafanya majaribio zaidi ya makombora yake.

Kundi hilo la mashambulizi la Marekani kwa jina Carl Vinson Strike Group linashirikisha meli ya kubeba ndege za kivita.

    Marekani: Hatutaivumilia tena Korea Kaskazini
    Wakazi Japan wajiandaa dhidi ya Korea Kaskazini

Lilitarajiwa kuelekea nchini Australia lakini badala yake likapelekwa magharibi mwa bahari ya Pacific ambapo hivi karibuni lilifanya mazoezi ya kijeshi na wanamaji wa Korea Kusini.

''Tutailaumu Marekani kwa matokeo mabaya yaliosababishwa na hatua yake'', ilisema taarifa hiyo ya wizara ya maswala ya kigeni ilionukuliwa na shirika hilo la habari la serikali KNCA.( chanzo BBC) 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE