April 13, 2017

KIKOSI KILICHOMUUA OSAMA CHATUMWA KUMWONDOA RAIS KIM JONG


Kikosi maalumu cha Kijeshi cha jeshi la Marekani kijulikanancho kama "Navy Seal Team Six" Kinadaiwa kujiandaa katika kumwondoa Kim Jong un wa Korea Kaskazini toka madarakani.
Navy Seal Team six ikishirikiana na wanajeshi wengine WATAALAAM wa vikosi vingine wamekuwa wakifanya Mazoezi kujitayarisha pindi watakapohitajika wakati wowote.
Kikosi hicho cha Navy Seal Team six ndicho kilichoweza kumuua Osama bin Laden baada ya kuingia nchini Pakistani usiku wa manane. Kikamuua yeye na walinzi wake na kuubeba mwili wake na kuutupa baharini.
habari kutoka gazeti la Australia na the Sun la Uingereza likinukuu habari za gazeti lingine la Korea Kusini Joog Ang newspaper likisema matayarisho ya kumwondoa Kim yako mbioni.
Hii inakuja wakati Marekani inafanya mazoezi makubwa ya WANAJESHI ZAIDI YA 17,000 wa ardhini
Angani
Maji 
na 
Nchi kavu 
pamoja na jeshi la Korea Kusini.
Maafisa wa serikali walipohojiwa walikanusha wakisema mazoezi hayo si ya kumwondoa Kim Jong Un.
Japokuwa well placeD sources zinasema mpango huo uko na waweza kutekelezwa wakati wowote ili kumzuia Dikteta huyo kumiliki zana hatari za Kinyukilia ambazo Marekani inadai Korea ya Kaskazini imo mbioni kutaka kuwa nazo.ili ziweze kuipiga Marekani. 
Nayo Marekani imesema haitairuhusu Korea ya Kaskazini kumiliki zana hizo. Ni juzi juzi tu wa kati rais Trump wa Marekani aliposema Anaweza kuchukuwa HATUA YEYE MWENYEWE bila msaada wa mtu mwingine.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE