April 22, 2017

KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU MTO RUAHA CHAINGIA SIKU YA TATU MKOANI MBEYA.

Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha kilichoko mkoani Mbeya kimeingia siku ya tatu kwa kutembelea sehemu mbalimbali na kufanya mahojiano na Wananchi na pia kutembelea maeneo  ambayo ni chanzo cha uharibifu wa maji ya mto Ruaha mkuu pamoja na  mazingira.
Katika siku ya tatu kikosi kazi kimekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo Wananchi kutokua na elimu ya matumizi ya maji ya mito ambapo wengi wao hutumia pampu kutoa maji kwenye mito  ili kupeleka maji kwenye mashamba yao pasipo wao kujua kuwa ni kosa. Mashamba mengi wilayani Mbalari yanatumia kilimo cha pampu kwa kuvuta maji toka kwenye mikondo ya mto Ruaha Mkuu  na kupeleka mashambani. Wakulima wa vitunguu, mahindi, mpunga, nyanya, mbogamboga na matunda.
Hutumia umwagiliaji wa aina hiyo. Pia hufanya ufyatuzi wa matofali kwa kutumia maji yaliyoko mtoni kwa kuyavuta kwa kutumia pampu. Wakiongea Wananchi wengi wamesema kuwa walikua hawajui kama.kufanya hivyo ni kosa kwa sababu hawana elimu ya kutosha katika hilo.
Wengi wanalima pembezoni mwa mito bila kuzingatia sheria ya mazingira isemayo Mkulima anatakiwa alime nje ya mita sitini kutoka mtoni. Kikosi kazi bado kipo katika  ziara yake Mkoani mbeya katika wilaya ya Mbalari. Kikosi kazi hiki kiliundwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania.
RUA13 (2)
RUA13 (1)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE