April 2, 2017

KASEJA SHUJAA WA LEO,SIMBA YAIPISHA YANGA KILELENI

Simba-vs-Kagera-Sgr
Na.Alex Mathias
Timu ya Simba imepunguzwa kasi kwenye mbio za ubingwa baada ya kutandikwa mabao 2-1 toka kwa Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
Alikuwa kinda wa Taifa Stars ambaye Simba walimlea Mbaraka Yusuph aliifungia Kagera Bao la uongozi dakika ya 27 kwa shuti kali lililomshinda Mlinda mlango wa Simba Daniel Agyei kwa makosa ya mabeki ambao walishindwa kujipanga vizuri.
Licha ya kufungwa Simba waliendelea kulishambulia lango la Kagera uzoefu wa Mlinda mlango Juma Kaseja umewafanya Simba kukosa ushindi kutokana na kuwa man of the Match kwa kuokoa michomo hatari hadi Mapumziko Kagera walikwenda wakiwa mbele 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote zilifanya mabadiliko na dakika ya 46 kinda wa zamani wa Simba tena Edward Christopher  alipingilia msumali wa pili kwa pasi nzuri ya Japhet Makalai.
Mzamiru Yassin alifunga bao la kufutia Machozi kwa Simba dakika ya 61 baada ya kutokea piga ni kupige kwenye eneo la Kagera Sugar hadi Mwamuzi anamaliza Mpira Kagera wameibuka na alama tatu muhimu.
Kwa Matokeo hayo Kagera Sugar wamefikisha pointi 45 na kuwashusha Azam FC kwenye nafasi ya tatu huku Simba wakibaki kwenye nafasi ya pili kwa alama 55 huku Yanga akishika usukani kwa alama 56.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE