April 19, 2017

KAMATI YA MBIO ZA MAGARI YAZUNGUMZA NA WANAHABARI IRINGA,DC KASESELA ATOA ONYO KWA WAZAZI

Ahmed Hueli kushoto ambae ni mkali wa mbio za magari
Mwenyekiti wa kamati ya mbio za magari mkoa wa Iringa Ahmed Mbata kushoto akizungumza na wanahabari leo leo katikati ni mkuu wa habari Iringa Richard kasesela 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wanahabari 

Serikali ya wilaya ya Iringa imewataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuchukua Tahadhari wakati wa mashindano ya mbio za magari.

Akizungumza Leo na wanahabari mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kwa siku ya jumamosi na junapili wakati mashindano hayo ya mbio za magari zilizodhaminiwa na kiwanda cha maji Mkwawa kuwa ni sehemu ya ukuaji wa uchumi wa mkoa

Alisema kuwa kiwanda hicho kimeonyesha uzalendo zaidi kwa kupitia maji hayo ambayo ni maji mapya.

Alisema kupitia mashindano hayo upo uwezekano mkubwa wa mkoa wa Iringa kuingia katika mashindano ya kimataifa ya mbio za magari.

Pia alisema kupitia mashindano hayo upo uwezekano mkubwa wa kutangaza hifadhi ya Taifa ya Ruaha .

Aidha alisema kuwa kwa wazazi wanapaswa kuwa makini na watoto pamoja na waendesha bodaboda kuacha kufukuza magari ya matangazo.

Mwenyekiti wa chama cha mbio za magari mkoa wa Iringa Ahmed Mbata alisema kuwa mkoa wa Iringa hadi sasa umeendelea kufanya vema kwenye mashindano hayo na upo uwezekano mkubwa wa kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mbata alisema kwa mkoa wa Iringa utawakilishwa na washiriki wawili akiwemo yeye na Mdhamini wa mashindano hayo Ahmad Hueli.

Kuwa washiriki 20 watashiriki mbio hizo na kuwa udhamini mkuu waemashindano hayo ni maji Mkwawa.

alisema washiriki wengine maarufu watashiriki mbio hizo.

Mwasisi wa mashindano hayo Francis Mwakatundu alisema kuwa Iringa ni tishio kwa mashindano hayo.
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE