April 16, 2017

ASKOFU DKT MDEGELLA ASEMA ASKOFU GWAJIMA NA BASHITE WANAJUANA VIZURI ,ATAKA WATANZANIA KUACHA KUPOTEZA MUDA

Askofu mteule wa kanisa la  Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa Blaston  Gavile (kulia)  akimpongeza askofu mstaafu wa dayosisi  hiyo Dkt. Owdenburg Mdegella baada ya  salam  zake za Pasaka kwa  waumini  wa usharika wa kanisa  kuu
Askofu  mteule  wa dayosisi ya  Iringa Blaston Gavile (kulia) na msaidizi  wake wakiongoza  ibada leo kanisa kuu
Mwalimu wa kwaya kuu Obed  Mella  akiongoza  kwaya yake  kuimba  wimbo la Haleluya kuu
Waimbaji  wa kwaya ya  vijana kanisa kuu
Waimbaji wa kwaya ya  vijana kanisa  kuu
waumini wa kanisa  kuu wakiwa ibadani
msaidizi  wa askofu dayosisi ya  Iringa
Askofu mstaafu Dkt  Mdegela  akiongea na mzee  Sanga 
Askofu  Dkt  Mdegella  akimpongeza  mwalimu wa kwaya kuu Obed Mella
Mwimbaji binafsi  akiimba  ibadani
Muumini wa  kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika  wa kanisa  kuu Onno Mella akipokea baraka za Pasaka jana toka kwa mkuu wa jimbo la  Iringa Mchungaji   Ambroce Mwakikoti nje ya  kanisa  hilo  baada ya  kumalizika kwa ibada ya  pili
Askofu mteule wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania ( KKKT)  dayosisi ya  Iringa Blaston Gavile kulia kulia na msaidizi wake Saga wakiongoza ibada leo kanisa kuu usharika wa kanisa kuu
Mwalimu wa kwaya kuu obed Mella akiongoza kwaya yake leo 
Kwaya ya vijana kanisa kuu wakiwa katika vazi maalum 
Waumini wa kanisa kuu wakiwa ibadani 
Waumini  wa KKKT  usharika wa kanisa  kuu  wakiwa  katika  ibada ya Pasaka  leo
Na MatukiodaimaBlog 
ASKOFU  (mstaafu)  wa kanisa la  kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT)  dayosisi ya  Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amesema   watanzania  wana mambo mengi ya  kufanya  ikiwa  ni pamoja na kujikita katika shughuli za  kiuchumi badala ya kupoteza muda  mwingi  kujadili  mambo  ya  Daud Bashite.

Akitoa  salama  za Pasaka  jana katika  usharika  wa kanisa kuu Dkt  Mdegella  alisema kuwa  watanzania wanapoteza  muda  mwingi kwa jambo hilo badala ya  kushughulika na mambo ya msingi yenye  tija kwa  Taifa .

“ Watanzania  wiki  tatu tunapoteza  muda kwa  habari za Bashite na Gwajima …hawa  wote  wametoka Mwanza  wanajuana  vizuri nawaombeni  watanzania  tusipoteze  muda bure  tujikite kwenye mambo ya  kiuchumi  mtu kama  amedandia  vyeti  atakamatwa  kwa  utaratibu  sasa  sisi  tumebaki  Bashite   Bashite yaani  ukitaka  kujua  nchi  hii  watu  wanapenda majungu angalia walivyokomalia hii la Bashite “

Alisema  Dkt  Mdegela  kuwa  watu  wanapoteza  muda  kushinda vijiweni  kuzungumia Bashite  badala ya  kwenda  kutafuta shughuli  za  kiuchumi kwa  ajili ya kupata fedha  .

Katika  hatua  nyingine  Dkt  Mdegella alipongeza kazi  nzuri  inayofanywa na Dayosisi    hiyo  chini ya  askofu mteule Blaston  Gavile kuwa heshima  kubwa  aliyoionyesha  kwa yeye kama askofu aliyeongoza kanisa hilo kwa  miaka 30  ya  kustaafu imekuwa ni  heshima  kubwa kwa kanisa  hilo ila mrithi  wake  anafanya  kazi  aliyomuachia vizuri  sana.

Hivyo  alishauri kanisa  hilo  kuanzisha baraza  la  wazee washauri nay eye  atakuwa  mwenyekiti wa  washauri  hao  ili  kulifanya kanisa   hilo  kuendelea  kufanya mazuri   zaidi.

Kwa  upande  wake askofu Mteule  wa  Dayosisi ya  Iringa katika  salam  zake  aliwataka  waumini  wa kanisa  hilo  kuendelea  kuuombea  mkoa  wa Iringa  na maeneo  mbali  mbali kuachana na matukio ya  ubakaji na ulawiti  ambayo yanazidi kuongezeka  siku hadi  siku .

“ Salam  zangu  kwenu  waumini ni  kuendelea  kuomba kwa ajili ya Taifa na mkoa wa Iringa tusema Mungu yatosha kuendelea  kusikia matukio ya ajabu ndani ya Taifa  letu …tuendelee  kuiombea nchi  yetu  kuwa ni ya amani  na kuepuka matukio yote ya utekaji na mauwaji kwenye    hili Taifa “

Alisema  Kanisa  limesikitishwa  sana  na mauwaji ya  askari  nane  waliouwawa  kinyama kwa  risasi na  kuwa kazi ya  wakristo isiwe  ya  kulalamika mitaani  kama  ilivyo kwa mataifa   kazi kubwa  iwe  ya  kufunga na kuomba kwa  ajili ya taifa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE