April 26, 2017

HIFADHI YA UDZUNGWA NI HIFADHI ISIYOTUMIKA KIKAMILIFU


Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoa Iringa Asia Abdalah akiwa na muongozaji watalii hifadhi ya milima ya Udzungwa wakijiandaa kupanda mlima udzungwa 

 Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah kushoto na wenzake wakitazama dawa ya kutibu magonjwa mbali mbali zikiwemo vidonda vya tumbo , meno ,tumbo na mengine ambayo inapatikana kwenye hifadhi ya milima ya milima ya Udzungwa 
 mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah akisaidiwa kupanda mlima Udzungwa
....................................
Na Francis Godwin wa matukiodaimablog na Gazeti la Mtanzania, Iringa 

ASILIMIA 80 isiyotumika vema ya Hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa ni jina la hifadhi wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa ikiwekewa mikakati ya kuvutia watalii itaongeza uchumi wa wilaya ya Kilolo yenye utajili mwingi ila watu wake ni masikini wa kipato .

Wahenga walisema mwenye kisu kikali ndie anayekula nyama hii ni sawa na jinsi ambavyo mkoa wa Morogoro wanavyofaidika na hifadhi hii ya Udzungwa kwa kuitumia vema asilimia yao 40 huku mkoa wa Iringa wenye asilimia 80 ya hifadhi hii wakibaki kuwa watazamaji wa sekta ya utalii .

Ifahamike kuwa hifadhi ya Udzungwa
inayopatikana katika bara la Afrika, nchini Tanzania, mkoani Morogoro, wilaya ya Kilombero asilimia na aslimia 80 Hifadhi hii ipo wilaya ya Kilolo ila ukosefu wa miundo mbinu umepelekea hifadhi hii kujulikana zaidi Upande wa Morogoro.

Jitihada za serikali ya wilaya ya Kilolo chini ya mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdalah na uongozi wa mkoa wa Iringa kupitia kwa mkuu wa mkoa Amina Masenza na kamati nzima ya utalii ni kuona hifadhi za mkoa wa Iringa ikiwemo Udzungwa zinajulikana na ndio maana ya kufunguliwa kwa lango la utalii wa kusini.

Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi lakini pia ubora wa barabara hifadhi hii ni jirani zaidi kuifikia iwapo utaingilia upande wa Lilli mkoani Iringa kwani hata idadi ya wanyama ni wengi zaidi Upande wa Iringa ila kwa utalii wa kutembea kwa miguu kuona maporomoko ya maji sanje ni upande wa Morogoro zaidi.

Jina la hifadhi limetokana na milima hiyo ya Udzungwa (yaani nchi ya Wadzungwa, tawi la Wahehe). 

Ina ukubwa wa kilometa mraba 1990, na ni hifadhi yenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote duniani.

Kati ya aina kumi na moja za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee .

"Mbega Mwekundu wa Iringa" (Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka 1979.

Kuna aina nyingine nne za ndege ambao hawakufanyiwa uchunguzi ambao ni: chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya iliyogunduliwa ya aina ya kwale wa Udzungwa zinazofanya hifadhi hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika. 

Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, chui, nyati na tembo.

"African violet" ni ua ambalo linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya miti mirefu inayofikia mita 30. Pia Mto Sanje ni kivutio kikubwa sana Mto huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa.

Faida kubwa kwa Udzungwa kwa mikoa yote na ukuzaji wa uchumi utaonekana zaidi iwapo Kilolo na mkoa wa Iringa kujipanga miundo mbinu ili kuvutia wawekezaji kujenga Hoteli za kitalii ambazo zitavutia watalii kugeukia kutembelea Udzungwa upande wa Kilolo Iringa.

Asia Abdalah mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambae ni mkuu wa kwanza wa wilaya Mwanamke kuonyesha nia ya dhati kwa kutaka lango la utalii hifadhi ya Udzungwa linafunguliwa Kilolo .

Anasema kuwa miundo mbinu bora itavutia watalii
zaidi kuwekeza wilaya ya Kilolo kwa kujenga hoteli za kisasa Udzungwa Wilayani Kilolo.

“Ndoto yangu kuona asilimia 80 za hifadhi hii zilizopo Kilolo zinakuza uchumi wa wana Kilolo na taifa kwa ujumla …nimetembea zaidi ya masaa 6 kupanda na kushuka mlima Udzungwa upande wa Kilombelo mkoa wa Morogoro hifadhi ya Taifa ya Udzungwa kuwa kuna maeneo mazuri ya wawekezaji kujenga hoteli ila hadi sasa bado changamoto ya hoteli inakwamisha watalii kufika Kilolo”

Asia anasema engo ya ziara yake hiyo ni kujifunza na kuona ni kwa kiasi gani hifadhi ya Udzungwa itanufaisha wananchi wa Kilolo kwa kupata wawekezaji zaidi.

Moja kati ya hifadhi yenye vivutio vizuri ni pamoja na Udzungwa ila changamoto kubwa ni uwekezaji kushindwa kujenga hoteli upande wa Kilolo na hivyo kuwepo kwa hoteli nyingi upande wa Kilombero kumetoa fursa kwa wananchi wa Kilombero kunufaika zaidi Jambo ambalo sasa linapaswa kuhamishiwa nguvu mkoa wa Iringa.

Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Dkt John Magufuli imekuwa mbele kuboresha mazingira ya uwekezaji hivyo kufunguliwa kwa uwekezaji wa Hoteli za kitalii Kilolo kutafungua uwekezaji wa viwanda mbali mbali.

“ Serikali yangu ya mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza imeweka mkakati wa kufungua lango la utalii mikoa ya kusini na tayari
Lango hilo limefunguliwa mwaka jana.”

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza anasema kuwa eneo la ujenzi wa kituo cha utalii
kwa mikoa ya Kusini kimetengwa eneo la Kihisa Kilolo mjini Iringa na kitapewa jina la karibu Kusini .

Tumekuwa na mikakati mbali mbali ya kuvutia utalii mikoa ya kusini baada ya muda mwingi utalii wa kusini kutojulikana na wengi wakiishia vivutio
vya utalii vya mikoa ya kaskazini pekee huku
hifadhi zetu nzuri za mikoa ya Iringa na mingine zikisaulika.

mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Udzungwa Hassan Nguluma anasema upo mkakati wa kuboresha miundo mbinu ya upande wa Kilolo ili kuvutia wawekezaji.

Kuwa hifadhi hiyo asilimia 20 ipo wilaya ya Kilombero na asilimia 80 ipo wilaya ya Kilolo ambako kuna wanyama wa kila aina huku upande wa Kilombero kuna maporomoko mazuri ya maji.

Kuhusu idadi ya watalii amesema kuwa wapo kutoka ndani ya nchi hasa wanafunzi na wageni toka nje japo changamoto kubwa kipindi cha masika ni ubovu wa miundo mbinu japo serikali ipo mbioni kuanza ujenzi wa Lami.

Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Dkt Allan Kijazi anasema kuwa mkakati wa kuvutia utalii mikoa ya
kusini umeanza na ili watalii wengi wapendelee
kufika hifadhi za kusini ni pamoja na kuboreshwa kwa miundo mbinu yake kikiwemo kiwanja cha ndege Nduli .

Anasema gharama kubwa ya nauli ya ndege
kutoka Dar es Salaam kuja Iringa ambayo ni sawa na nauli ya kutoka Dar es Salaam kwenda Dubai inawafanya watalii kutopenda kuja mikoa ya
Kusini hivyo iwapo uwanja wa Ndege utaboreshwa na ndege kutua kwa wingi watalii wengi
watatembelea hifadhi hizo .
MWISHO

Mwandishi anapatikana kwa simu 0754026299 barua pepe ; francisgodwin2004@yahoo.com

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE