April 7, 2017

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA YANGA

Siku chache baada ya mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma kuanza mazoezi hatimaye kuna habari nzuri kwa klabu ya Yanga baada kiungo Thabani Kamusoko naye kuaanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya MC Alger ya Algeria.
Kamusoko amesema, anataka kujaribu bahati yake kwani anajisikia nafuu baada ya kupata matibabu kutoka kwa jopo la madaktari wa timu hiyo.
“Najisikia nafuu kiasi na ndiyo maana nimerudi uwanjani kwa ajili ya kuangalia kama nitaweza kuisaidia timu yangu kwenye mechi zilizosalia ikiwemo mchezo wa Jumamosi dhidi ya MC Alger,” amesema Kamusoko.
Nyota hao wawili raia wa Zimbabwe walikuwa nje kwa muda kutokana na kuuguza majeruhi ambayo yamewafanya kukosa mechi kadhaa ikiwemo mchezo uliopita dhidi ya Zanaco na ule wa ligi ya Vodacom dhidi ya Azam FC.
Daktari  wa timu hiyo, Edward Bavu, amesema wachezaji wake majeruhi wote wamepona na wameanza mazoezi isipokuwa mgonjwa mpya Mzambia, Justine Zulu aliyeumia katika mechi dhidi ya Azam FC.
Bavu amesema, Zulu yeye jana Jumanne asubuhi alitarajiwa kupeleka hospitali kwa ajili ya kusafishwa kidonda chake kabla ya kutolewa nyuzi na kuanza mazoezi mepesi.
"Ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga kusikia wachezaji wetu ambao ni muhimu kwenye timu wakirejea uwanjani katika mechi muhimu ambayo tunahitaji ushindi katika uwanja wetu wa nyumbani.
“Ngoma na Kamusoko wamepona majeraha yao na leo Kamusoko ameanza mazoezi mepesi ya binafsi, baada ya kumaliza programu ya gym na matibabu yake.
"Niseme kuwa, wachezaji hao wapo chini ya uangalizi kwa siku hizi mbili kabla ya kuanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzao katika kujiandaa na mechi na Alger,” amesema Bavu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE