April 5, 2017

DC KILOLO AKUTANA NA MAPACHA WALIOUNGANA WAMPA UJUMBE KWA AJILI YA RAIS DKT MAGUFULI

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah kulia akifurahi na watoto mapacha walioungana  wakazi wa Makete wanaoiahi Kilolo 
Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mlezi wa mapacha hao 
MAPACHA waliozaliwa wameungana Consolata na Maria mwakikuti wazaliwa wa Makete mkoa wa Njombe ambao wanaendelea na masomo wilayani Kilolo mkoa wa Iringa watoa ujumbe mzito kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah. 

Mapacha hao walimweleza jana mkuu wa wilaya ya Kilolo aliyetembelea kituo wanacholelewa kuwa azidi kufanya kazi ya kuwatumikia wana Kilolo kwa kuwakumbuka  yatima wengine. 

Kuwa wapo yatima wanaoteseka kwa kukosa msaada huku baadhi ya jamii ya Kilolo ikipata tabu ya huduma ya afya hivyo kuomba serikali kuzidi kuboresha huduma za afya vijijini. 

Kuhusu jitihada zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli mapacha hao walimwomba mkuu huyo wa wilaya kufikisha salamu zao za pongezi na kuomba kuendelea kuwatumikia kwa kasi hiyo watanzania. 

Hata hivyo waliomba serikali kuendelea kuboresha elimu mashuleni kwa kutatua changamoto ya vitabu vya sayansi ili kuzalisha wasomi zaidi wa masomo ya Sayansi nchini. 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo alisema kuwa serikali inawathamini na inaendelea kuwapenda hivyo kama mkuu wa wilaya ataendelea kufika kuwasalim na kuwasaidia. 

"Nimefurahi sana kuwaona mkiwa na furaha kubwa na mnafanya vema katika msomo yenu kwa kufanya vizuri katika msomo yenu ya kidato cha nne na sasa wapo kidato cha sita "

Alisema kuwa watoto hao mapacha wanaonyesha matumaini makubwa ya kwenda chuo kikuu kutokana na jitihada zao darasani na kuwa wanafanya vizuri masomo yao ya kidato cha sita sasa. 

Mapacha hao walizaliwa mwaka 1996 kijiji cha Ikonda wilaya ya Makete mkoani Njombe walipata elimu yao ya msingi kijijini hapo na kufanikiwa kufaulu vizuri kabla ya mwaka 2011 kuchukuliwa kwa malezi na wamisionari hao na kuletwa wilayani kilolo kwa ajili ya kuwalea zaidi. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE