April 6, 2017

DC MUFINDI ATEKETEZA JARUBA ZA BANGI, WATATU WAKWEMO VIONGOZI WA KIJIJI NA MZEE WA KANISA WAKAMATWA

mkuu wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Jamhuri Wiliam Kushoto akiongoza  kamati ya ulinzi na usalama wilaya kuteketeza bangi. 
Kamati ya ulimzi na usalama wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa wakiteketeza shamba la bangi 

Askari wakifyeka shamba la bangi 
Watuhumiwa wa kilimo cha bangi 
DC Mufindi akiwa katika msako wa bangi 
MKUU wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Jamhuri Wilim leo ameendesha msako wa wananchi wanaojihusisha na kilimo cha bangi kwenye misitu ya kijiji Cha Ihanganatwa na kisada   tarafa ya Malangali halmashauri ya mji Mafinga na kuteketeza mashamba ya bangi iliyolimwa kwenye misitu hiyo. 

Katika tukio hilo mkuu huyo wa wilaya ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya aliongozana na kamati yake pamoja na mkurugenzi wa halmashauli ya mji Mafinga .

Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima eneo la tukio mkuu huyo wa wilaya alisema bangi hiyo ambayo imefyeka na kuteketezwa kwa moto ilikuwa imelimwa katika maeneo matatu tofauti yaliyochomewa mkaa ila eneo moja bangi hiyo ilifyekwa na watuhumiwa kwa lengo la kupoteza ushahidi. 

Alisema watuhumiwa watatu wamekamatwa kuhusika na kilimo cha bangi akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha  Ihanganatwa, Enock Mkela na mzee wa kanisa la Sabato Joshua Mlowe pamoja na kaimu afisa mtendaji wa kijiji ambae ni afisa kilimo kijiji cha Ihanganatwa Antony Mwambene kwa kushindwa kubaini kilimo hicho. 

Mkuu huyo alisema taarifa za kuwepo kwa watu wanaojihusisha na kilimo cha bangi katika tarafa hiyo zimefikishwa na raia wema na kuwa msako kwenye wilaya nzima ya Mufindi umeanza na wote watakamatwa. 

"Tunataarifa za wote wanaolima bangi na hatutalala tutaifanya kazi hiyo usiku na mchana "

Mkuu huyo alisema utekelezaji wa agizo la mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa mkuu wa mkoa Amina Masenza linafanyika kwa makini na hawatakubali Wilaya ya Mufindi kuwa nyuma kutekeleza agizo hilo ambalo limetolewa na Rais Dkt John Magufuli kwa viongozi wote. 

Alisema mwenyekiti huyo wa kijiji amekamatwa kutokana na kosa la kushirikiana na mtuhumiwa ambae ni mdogo wake kabla ya kumtorosha kuvuna na kuficha ushahidi wa bangi aliyotakiwa kulinda kama ushahidi .

Hata hivyo mapema mkuu wa mkoa wa Iringa ambae alikusudia kuongoza zoezi hilo la kwanza mkoani Iringa kuteketeza bangi alisema kuwa ofisi yake inayotaarifa za kutosha za wakulima wa bangi na kuwataka kujisalimisha. 

Huku akiwapongeza wananchi kwa kuendelea kufichua wote wanaolima bangi

kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi amesema jeshi Lake litaendelea na mapambano ya dawa za kulevya. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE