April 8, 2017

DC KILOLO AFANYA ZIARA YA KWANZA HIFADHI YA TAIFA UDZUNGWA ASHAURI WAWEKEZAJI KUWEKEZA UPANDE WA KILOLO

mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa Asia Abdalah akijiandaa kuanza ziara ya kuhamasisha utalii wilaya ya Kilolo kwenye hifadhi ya Udzungwa leo 
maporomoko ya mji ya Sanje Udzungwa ambayo ni kivutio kikubwa 
mwanahabari Augustino Kihombo akipanda mlima Udzungwa
 Zoezi la kupanda Mlima Udzungwa
Mwongoza wageni Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa akimsaidia mkuu wa Wilaya Kilolo Asia Abdalah kupanda mlima 
Mkuu wa Wilaya Kilolo Asia Abdalah akizungunza watalii toka nje ya Tanzanian waliotembelea hifadhi ya Udzungwa
Mkuu wa wilaya akimbusu mtoto aliyepanda mlima Udzungwa na wazazi wake 
Hapa wakitazama majani ambayo ni dawa ya kutibu jino na tumbo

Mzee wa matukiodaima mwenye bendera ya Taifa akiwa na wadau pamoja na DC kilolo
Barabara ya Kilombero ni changamoto kwa utalii Udzungwa 
DC Kilolo akila nyama ya dafu
Mzee wa matukiodaima akiwa na mmoja kati ya watalii wa nje 
MKUU wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah amefanya ziara ya kikazi katika hifadhi ya Taifa ya  Udzungwa upande wa Kilomboro mkoani Morogoro na kuomba wawekezaji wa hoteli za kitalii kujitokeza kuwekeza upande wa kilolo. 

Alisema hifadhi ya Taifa ya Udzungwa kwa zaidi ya asilimia 60 ipo wilaya ya Kilolo na kuna maeneo mazuri ya wawekezaji kujenga hoteli ila hadi sasa bado changamoto ya hoteli inakwamisha watalii kufika Kilolo. 

Hivyo alisema lengo ya ziara yake hiyo ni kujifunza na kuona ni kwa kiasi gani hifadhi ya Udzungwa itanufaisha wananchi wa Kilolo kwa kupata wawekezaji zaidi. 

Alisema kuwa kwa upande wa kilolo kuna eneo kubwa la hifadhi na kuna wanyama wengi zaidi iwapo hoteli zitajengwa watalii wengi watapenda kutembelea hifadhi hiyo.

Kwani alisema moja kati ya hifadhi yenye vivutio vizuri ni pamoja na Udzungwa ila changamoto kubwa ni uwekezaji kushindwa kujenga hoteli upande wa Kilolo na hivyo kuwepo kwa hoteli nyingi upande wa Kilombero kumetoa fursa kwa wananchi wa Kilombero kunufaika zaidi Jambo ambalo sasa linapaswa kuhamishiwa nguvu mkoa wa Iringa. 

Alisema serikali ya awamu ya nne chini ya Rais  Dkt John Magufuli imekuwa mbele kuboresha mazingira ya uwekezaji hivyo kufunguliwa kwa uwekezaji wa Hoteli za kitalii Kilolo kutafungua uwekezaji wa viwanda mbali mbali. 

Aidha alisema tayari serikali ya mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza imeweka mkakati wa kufungua lango la utalii mikoa ya kusini na tayari 
Lango hilo limefunguliwa mwaka jana. 


Wakati huo huo mkuu huyo wa wilaya wa kwanza mwanamke kupanda mlima Udzungwa kwa masaa zaidi ya manne kwenda kileleni ametajwa kuwa ni mkuu wa wilaya wa kwanza mwanamke kupanda mlima huo kwa haraka zaidi ukilinganisha na wanawake wengine. 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE