April 13, 2017

BILIONI SABA ZATUMIKA KULIPIA FIDIA NA SHUGHULI ZA KUWAHAMISHA WANANCHI IHEFU BILA MAFANIKIO

Mkurugenzi mkuu wa Tanapa Dkt Allan Kijazi akitoa taarifa ya mto Ruaha mkuu  kwa makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha
mwonekano wa mto Ruaha mkuu baada ya maji kutofika 
.....................................................
Na MatukiodaimaBlog 

SHIRIKA la hifadhi ya Taifa ( TANAPA)  limedai kumia kiasi cha Shilingi bilioni saba kulipa fidia na gharama nyingine kunusuru bonde la usangu kwa ajili ya mto Ruaha mkuu bila mafanikio. 

mkurugenzi mkuu wa TANAPA Dkt Allan Kijazi alimweleza jana makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan baada ya kutembelea hifadhi ya Ruaha kutembelea mradi wa uhifadhi wa Ikolojia kwenye mto Ruaha mkuu. 

Alisema kuwa mbali ya shirika kutumia kiasi hicho kikubwa cha pesa kulipa fidia kwa ajili ya kunusuru mto Ruaha mkuu lakini bado zipo changamoto zinazoathiri usimamizi wa eneo na zinahitajika uamuzi wa serikali. 

Dkt Kijazi alisema shirika lake linapongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Jonh Magufuli kwa kuomyesha ushirikiano mkubwa wa kusimamia hifadhi ya mazingira na Raslimali kwa ujumla. 

"Tunaimani kuwa kwa jitihada hizi tunaweza kuboresha mazingira na viumbe kwa manufaa mapana ya kizazi cha sasa na kijacho "

Hivyo alisema ombi la shirika kwa makamu wa Rais na serikali kwa ujumla kuzidi kusaidia katika kunusuru bonde la usangu ili liweze kurejesha mtiririko wa maji kwa ajili ya matumizi ya hifadhi ya Ruaha, mabwawa ya Mtera na kidato na pia kwa ajili ya matumizi ya wananchi wengine walio katika maeneo ya chini ya mkondo wa maji ya mto Ruaha. 

Kuwa mikakati ya uhifadhi wa mto Ruaha iende sambamba na kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi na wananchi ambao umedumu kwa miaka takribani kumi sasa toka mwaka 2008 mkoni Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE