April 13, 2017

AMWAMBUKIZA UKIMWI BINTI YAKE KWA MAKUSUDI


Musoma. Binadamu wamejivalisha roho ya ushetani, hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea tukio la baba mzazi tena muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi kumbaka binti yake.
Kutokana na kitendo hicho, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Musoma, Karim Mushi amemhukumu mkazi wa Kijiji cha Baranga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Nyamahemba Chacha (46) kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake na kumsababishia maambukizi ya Ukimwi.
Akitoa hukumu hiyo juzi, Hakimu Mushi alisema Mahakama imeridhishwa pasi na shaka na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mshtakiwa.
Akirejea ushahidi huo, Hakimu Mushi alisema Novemba 30, 2016 saa tatu usiku, mshtakiwa aliingia kwenye chumba cha watoto wake na kumuita binti yake akimweleza anaitwa na kaka yake.
Alisema baada ya mtoto huyo kutoka alimkamata na kumuingiza chumbani kwake na kumpa vitisho, alimwingilia kimwili, licha ya kutambua kuwa anaishi na VVU.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE