April 27, 2017

ALPHONCE SIMBU APOKELEWA KWA SHANGWE BUNGENI


SIMBUMwanariadha Alphonce Simbu aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya London Marathon atembelea bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Alhamisi April 27 akiwa ni mgeni maalum wa Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Harison Mwakyembe. Baada ya kutembelea bunge hilo Simbu pia atakuwa na mazungumzo na Waziri Mwakyembe.
Simbu ataambatana na muwakilishi wa wadhamini wake DStv pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT.
Akizungumzia mualiko huo, mwanariadha huyo amesema kuwa amefurahi sana kupata mualiko wa Waziri anayehusika na sekta ya michezo kwenda bungeni kama mgeni wake maalum. Amesema hii inaonyesha kuwa serikali inatambua jitihada zake anazozifanya katika kuiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa. “Nimefurahi sana kualikwa na muheshimiwa Waziri kumtembelea bungeni, bila shaka hii itakuwa fursa nzuri ya hata wabunge kutambua jitihada tunazofanya vijana wao katika kuliletea taifa sifa. Natumaini pia nitapata fursa ya kuongea ana kwa ana na Waziri” alisema Simbu na kuongeza kuwa atatumia fursa hiyo kumueleza Waziri changamoto nyingi wanazokabiliana nazo wanamichezo hapa nchini.
Amesema kuna mengi ya kuongea na Waziri na kwamba anaamini mazungumzo yao yatakuwa na tija na manufaa si kwake tu, bali kwa wanamichezo wote kwa ujumla.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana, ambaye anaandamana na Simbu, amesema kuwa anaamini kuwa ziara hiyo na mkutano na Waziri utakuwa na manufaa makubwa kwani pia itakuwa ni fursa nzuri ya kujadili namna bora zaidi ya Serikali kushirikiana na wadau katika kuimarisha na kuendeleza michezo hapa nchini. “sisi kama wadhamini wa mwanariadha huyu tunaamini kuwa kitendo cha Waziri kutualika ni ishara tosha kuwa kweli anadhamiria kushirikiana na sisi wadau wa michezo ili kuongeza nguvu za pamoja za kuimarisha michezo hapa nchini” alisema Mshana
Multichoice Tanzania kupitia DStv imekuwa ikimdhamini Simbu tangu mwaka jana na udhamini huo pia umewanufaisha wanariadha wengine ambao wamekuwa kambini kwa muda sasa pamoja na simbu. “Kambi ya mazoezi ya Simbu ambayo ilidhaminiwa na DStv pia ilikuwa na wanariadha wengine ambao wote walinufaika moja kwa moja na udhamini huo. Tunaamini kuwa pia kati ya hao tutapata wanariadha watakaofanya vizuri siku zijazo”.
Alphonce Simbu, ambaye pia ni mshindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Mumbai Marathon ni miongoni mwa wanariadha wa timu ya Taifa itakayoshiriki katika mashindano ya Dunia yatakayofanika jijini London  mwezi Agosti mwaka uu

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE