April 12, 2017

AIBU MKOA WA IRINGA KUWA NA UDUMAVU -MAKAMU WA RAIS SAMIA

Makamu wa Rais Samia suhulu Hassan
makamu wa Rais akiwa picha ya pamoja na kikosi kazi 
Makamu wa Rais akiwa na wakuu wa wilaya 
MAKAMU wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan asema ni aibu kwa mkoa wa Iringa unaoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kuwa na kuwepo katika orodha ya mikoa inayoongoza kwa utapiamlo .
Akizungumza na viongozi mbali mbali wa mkoa
wa Iringa mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Iringa kutoka kwa mkuu wa mkoa huo Amina Masenza ,makamu wa Rais alisema kuwa mkoa wa Iringa umeonyesha kufanya mambo mengi mazuri likiwemo la kilimo na uzalishaji wa mazao ya chakula ,ukusanyaji wa mapato,kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba kwa kuwa mkoa mmoja kati ya mikoa 10 bora ila mkoa huo unatia aibu katika eneo la utapiamlo na UKIMWI.
“Nawapongezeni sana viongozi wote wa mkoa wa Iringa mnafanya kazi nzuri sana ya kutekeleza maagizo mbali mbali ya kitaifa yanayotolewa na Rais wetu Dkt John Magufuli …kweli mpo juu sana name nawapongeza sana ila siwezi kuwasifia kwa aibu hii ya watoto kuwa na udumavu kwa kukosa
lishe bora na hili la UKIMWI”
Makamu wa Rais alisema kwa kuwa lengo la ziara
yake hii mkoa wa Iringa kwa sasa ni kunusuru mto Ruaha mkuu usitoweke anakusudia kupanga ziara
rasmi ndani ya mkoa wa Iringa ambayo atazunguka mkoa mzima na kutazama sekta moja
hadi nyingine ili kuweka mkakati wa kutatua
changamoto ambazo zinaukabili mkoa ikiwemo ya udumavu kwa watoto.
Katika hatua nyingine makamu wa Rais amepingana na tafiti ya kuwa watanzania tunaishi chini ya dola moja na kuwa watanzania tuna uwezo wa kula matunda zaidi ya matatu na kuwa tunaishi kitajiri zaidi japo umasikini wetu ni wa kujitakia.
Kuhusu fedha za mfuko wa TASAF zinazotolewa kwa familia zisizo na uwezo makamu wa Rais aliwataka viongozi wa mkoa wa Iringa kusimamia
utaratibu huo na kuwa wanaopata fedha hizo wawe kweli walengwa na isiwe kama mkoa wa Arusha ambao umetoa fedha hizo kwa watu ambao si walengwa
Alisema kuwa fedha hizo ni fedha za wahisani
na ni vema zitumike vizuri kwani ni fedha ambazo
zitakuja rejeshwa na vizazi vijavyo hivyo lazima
utaratibu utumike kutoa fedha hizo
Akielezea kuhusu suala la nishati ya umeme alisema kuwa hadi mwaka 2020 serikali ya awamu ya tano imekusudia kuona vijiji vyote nchini
zinapatiwa umeme na hakutakuwa na kijiji kisicho na umeme .
Wakati huo huo makamu wa Rais amepongeza kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa kwa kazi nzuri ya kuufanya mkoa huo kuwa salama.
Huku akiwataka wananchi kutoa taarifa mapema za kuwatumbua wale wote wanahisiwa ni waarifu.
Awali akitoa taarifa ya mkoa ,mkuu wa mkoa wa Iringa Masenza alisema kuwa hali ya lishe kwa
watoto chini ya miaka mitano sio ya kuridhisha ,kwani kulingana na matokeo ya utafiti wa lishe wa mwaka 2014 kiwango cha udumavu kwa mkoa wa Iringa kilikuwa asilimia 51.3 ,ukondefu asilimia 0.2 na uzito pungufu asilimia 15.5 kuwa sababu kubwa ya utapiamlo katika mkoa ni lishe duni kutokana na waqnanchi kutokuwa na elimu ya utoaji wa chakula cha kutosha na chenye mchanganyiko wa viini lishe na sababu nyingine mbali mbali zikiwemo za magonjwa kama malaria ,kuharisha ,kichomi na UKIMWI.
Makamu wa Rais yupo mkoani Iringa kwa ziara ya
siku nne itakayomalizika kesho ziara ya kunusuru
mto Ruaha mkuu unategemewa na watu zaidi ya
milio 6 kwa kuunda kikosi kazi cha Taifa kwa ajili ya usimamizi uhifadhi wa Ikolojia kwenye mto
huo

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE