March 10, 2017

WINNIE MANDELA NI MGONJWA ALAZWAAliyekuwa mke wa shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela, amelazwa hospitalii kwa kile kinachotajwa kuwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Familia yake inasema kuwa alipelekwa hospitali ya Milpark mjini Johannesburg.

Mwezi Disemba mwaka uliopita, Bi Madikizela-Mandela alilazwa hospitali hiyo lakini kile kilichosababisha alazwe hakikutajwa.

    Winnie Mandela aukosoa uongozi wa ANC
    Winnie Mandela aibiwa dola 6000 kutoka nyumbani kwake
    Raia wa Malawi na DRC miongoni mwa wanawake 100 wa BBC

Msemaji wake Victor Dlamini, aliambia BBC kuwa alikuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida lakini madaktari wakaamua kumlaza.

Bi Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela, na alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kusajiliwa kama mhudumu wa kijamii nchini Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE