March 16, 2017

WAZIRI WA AFYA AAGIZA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA KUCHUNGUZWA , ASEMA MADAKTARI NA WAUGUZI WAZEMBE KUFUTIWA LESENI

waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akipata  taarifa ya  afya  mkoa  wa Iringa katika  ofisi ya  mkuu wa mkoa kabla ya  kufanya ziara  yake Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa leo
Mganga  mkuu  wa mkoa wa Iringa  akisoma taarifa ya  afya  mkoa huo  mbele ya waziri wa afya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akizungumza na  viongozi wa mkoa wa Iringa leo  kulia wa  pili ni mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na  kushoto ni katibu tawala wa mkoa Wamoja Ayubu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akipokelewa na  watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa
Wauguzi  Hospitali ya  mkoa wa Iringa  wakimpokea waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu
Msafara  wa  waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu ukitembelea  kituo cha damu  salama  kilichojengwa na kampuni ya Asas Ltd ya mkoani Iringa  kwa kiasi cha Tsh milioni 250
Waziri wa afya  akipata maelezo ya  kituo cha damu salama
Waziri Ummy akitoa maelekezo kwa msimamizi wa  kituo cha damu  salama  Iringa
Waziri  wa Afya  Ummy Mwalimu  akifurahi na mtoto  aliyelazwa katika  wodi la  watoto waliozaliwa kabla ya muda  wao watoto njiti ambae  sasa anaendelea  vizuri
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akiagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuchunguza Hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa kwa  kukosa  dawa  wakati  serikali imeipatia kiasi cha Tsh milioni 160 za dawa ,kutoka  kulia ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akisisitiza  jambo  wakati wa ziara  yake hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa  leo
waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akisalimiana na  watumishi  wa Hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa  leo
Watumishi  Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi wakimpokea  waziri wa afya
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akitoa maelekezo eneo la mapokezi katika Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi leo
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akifurahi jambo na wazazi waliotoka kujifungua katika  hospitali ya  wilaya ya Mufindi  leo
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu akitembelea  Hospitali ya  wilaya ya Mufindi
WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ummy Mwalimu ameagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi wa tatizo la uhaba wa dawa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Kuwa haiwezekani serikali ya Rais Dkt John Magufuli kuongeza pesa za dawa kutoka milioni 110 awali hadi milioni 160 ila bado wagonjwa wananunua dawa katika maduka binafsi.

Waziri huyo alitoa agizo hilo leo  wakati wa ziara yake katika Hospitali hiya, kuwa ameshangazwa kusikia malalamiko toka kwa ndugu wa wagonjwa kuwa dawa wanaelekezwa kwenda kununua duka binafsi la Miyomboni.

Alisema kuwa sehemu kubwa ya maduka hayo ni mali ya watumishi wa Hospitali ama marafiki zao na ndio sababu inayopelekea kuwaandikia dawa zilizopo kwenye maduka hayo .

"mkisikia siku nimetumbuliwa na Rais Dkt Magufuli basi ni kutokana na hii vita ninayokwenda nayo ya kubanana na bohari kuu ya dawa (MSD)... na sipo tayari kuona natumbuliwa kwa ajili ya MSD haiwezekani jitihada hizi kubwa za serikali watu wachache wakaturudisha nyuma "

Waziri huyo aliagiza kila hospitali ya rufaa ya mkoa kuwa na duka lake la dawa ili kuwawezesha wagonjwa kununua dawa za bei ya kawaida.

Alipongeza mkoa wa Iringa kwa kuanza ujenzi wa duka hilo na kushauri mara litakapo kamilika kuanza kazi haraka.

Hata hivyo alisema kwa upande wake na makamu wa Rais mama Samia Suhulu wameelekeza nguvu zao katika uboreshaji wa huduma ya mama na mtoto na pindi atakapo ondoka madarakani basi atataka kukumbukwa kwa kazi hiya.

Aidha aliagiza wakurugenzi kote nchini kuwalipa pesa za ununuzi wa sare wauguzi wote nchini na kuwa suala hilo si ombi ni lazima.

Alisema kuwa kuwa wauguzi ndio kiungo muhimu kati ya madaktari na wauguzi na kuwa suala la vifaa limeanza na lengo la serikali kuboresha hadhi ya hospitali hizo za rufaa mkoa ili kuwa na ubora stahiki.

Katika hatua nyingine waziri huyo amepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na wadau katika kuboresha mazingira ya hospitali hiyo na kuwa msaada wa Milioni zaidi ya 500 uliotolewa na familia ya mfanyabiashara Salim Asas kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo cha damu salama naununuzi wa vifaa na ule wa wodi ya watoto wanaozaliwa kabla ya siku zao (Watoto njiti) ni msaada mkubwa ambao serikali imeupokea kwa mikono miwili na kutaka wadau wengine kusaidia.

Waziri Mwalimu alisema Kwa ajili ya kuboresha zaidi hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Iringa aliagiza mchakato wa ujenzi wa wodi la wagonjwa wa dharula kuanza na kuwa wizara yake itaanza kupita hospitali zote za rufaa kwa ukaguzi ikiwa ni pamoja na kuziwekea alama hospitali zisizo chini ya kiwango.

Kuwa kutokana na eneo la hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Iringa kubanwa na ofisi za TANROADS ambao tayari wamehamisha ofisi zao kupisha upanuzi wa hospitali hiyo, kuwa bado ataendelea kuzungumza na waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba ili gereza kuu la Iringa kuhamishwa haraka eneo hilo.

Wakati huo huo waziri Mwalimu amesema kuwa madaktari na wauguzi wasiotimiza wajibu wao watawajibishwa.

"sijasema kuwa msiguswe nimesema wapo wachache wenu ambao hamtimizi wajibu wenu...mimi nileteeni muuguzi mmoja au daktari mmoja ambae amekwenda kinyume na maadili ya kazi yake nitamfutia leseni yake, naomba ijulikane wazi kuna vitu viwili kama umekiuka maadili yako nitashughlika nawe ila kama umeiba dawa ruksa wakuu wa mikoa ama wilaya kushughulika nanyi "waziri Ummy aliwataka wauguzi na madaktari wote nchini kutimiza wajibu wao ili wasiguswe.

Picha  zote na habari na  matukiodaimaBlog

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE