March 16, 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA

waziri  wa afya  Ummy  Mwalimu  akitoa maelekezo kwa uongozi wa  Hospitali ya  wilaya ya Mufindi  kuboresha  eneo la mapokezi kwa  kufunga mashine ya  kietroniki kwa ajili ya kufanya malipo
Waziri  Ummy  Mwalimu  akitembelea  Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi  leo
Waziri Ummy  akiwa katika  picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya wilaya ya  Mufindi
Wodi  la  watoto njiti  lililojengwa na kampuni ya Asas  Ltd ya  Iringa kwa  zaidi ya Tsh milioni 350
Waziri wa Afya  akitembelea  wagonjwa
Mganga  mkuu wa mkoa  wa Iringa akitoa taaarifa ya afya mkoa
Waziri wa afya  Ummy Mwalimu  akimtazama mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  wakati akimsisitiza mwanamke kumlisha mtoto wake lishe  bora  uji wa dona
Waziri wa Afya  akimsikiliza mmoja kati ya   madaktari wa  Hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Iringa

- Aagiza kuanzishwa duka la Dawa ndani ya miezi 3.

- Ataka wajenge Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura (Emergency Unit)
- Aagiza Hospitali zote za Mikoa na Wilaya kuanzisha Wodi za Watoto Wachanga na Watoto Njiti ndani ya kipindi cha miezi 6.Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa leo tarehe 16/3/2017 ambapo ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kituo cha  Damu Salama cha Mkoa pamoja na Hospitali ya wilaya ya Mafinga. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utoaji wa huduma za Afya kwenye vituo vya umma Afya hapa nchini

Akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za Afya katika mkoa mbele ya Waziri wa Afya, mhe. Amina Masenza, mkuu wa Mkoa wa Iringa alieleza hatua mbalimbali wanazochukua katika kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo vya Afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na lishe kwa wananchi bila kusahau kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Hata hivyo, zipo changamoto kadhaa zinazowakabili mkoa kufikia lengo la lao kutoa huduma bora za Afya.

 Mathalani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Iringa haina wodi/kitengo cha dharura, upungufu wa watumishi, Ufinyu wa eneo la Hospitali, ukosefu wa Gari la Kubebea Wagonjwa na ukosefu wa baadhi ya vitendanishi.

Mhe.Ummy Mwalimu amewapongeza viongozi na watumishi wa mkoa kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuboresha huduma za afya ikiwemo kufanikisha ujenzi wa wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati na watoto wachanga.

Wodi hiyo yenye vifaa vyote muhimu imejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya ASAS ya Mjini Iringa. Mhe Ummy amewataka wadau wengine waendelee kusaidia sekta hii hususani eneo la Afya ya Mama na Mtoto kwa kuwa linawagusa wananchi wengi hasa wa kipato cha chini.

Kufuatia malalamiko aliyoyapokea kutoka kwa wananchi waliofika kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Mhe.ummy aliagiza utekelezaji wa masuala yafuatayo; ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa dharura na duka la dawa la Hospitali ili kuondoa usumbufu wanaoupata wagonjwa wa kwenda kununua dawa kwenye maduka binafsi.

Pia,aliahidi kulifuatilia suala linalohusu gereza lililopo jirani na Hospitali ya mkoa ili liweze kuhamia sehemu nyingine na kutoa eneo kwa Hospitali.

Vile vile, ametoa muda wa miezi 9 kuanzia leo tarehe 16 March kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha vituo vyote vya Afya vinatoa huduma kamili za uzazi za dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni.

Akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi, mhe. Ummy aliagiza yafuatayo; uongozi wa wilaya uhakikishe maji yanapatikana muda wote hospitalini, waanzishe ndani ya mwezi mmoja wodi maalum kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na Watoto wachanga.

Pia, aliwakumbusha juu kuhakikisha kuwa wazee wote wanatambuliwa na kupewa vitambulisho lakini alipongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya kuwakatia Wazee kadi za Bima (TIKA).

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE