March 21, 2017

WAZIRI PROF MUHONGO AZINDUA MRADI WA UMEME WA REA AWAMU YA TATU KILOLO, ASEMA HADI 2021 VIJIJI VYOTE NCHINI KUWA NA UMEME

Waziri Wa Nishati na Madini Prof Sosipeter Muhongo wa pili kulia akisomewa bando na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto leo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa Rea 
Waziri Prof Muhongo akiunganisha waya kubonyeza King'ora kuzindua mradi wa umeme
Waziri Prof Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Iringa na makandarasi watakaotekeleza mradi wa Rea awamu ya tatu mkoa wa Iringa 
mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akisoma taarifa ya mkoa
Waziri Muhongo akimpongeza mwanafunzi wa sekondari ya wasichana jamii ya kimasai kwa shairi zuri
Mbunge wa kilolo wa pili kushoto akicheza wakati wa kwaya ya wanafunzi wa kike jamii ya kimasai wakiimba
Waziri Muhongo kisalimiana na viongozi mbali mbali


Waziri wa Nishati na Madini Prof Sosipeter Muhongo amezindua mradi wa Rea awamu ya tatu katika mkoa wa Iringa huku akimpongeza mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto kwa kuwapigania wananchi wake kupata umeme. 

Akizindua mradi huo Leo katika kijiji cha Image wilaya ya Kilolo Waziri Prof Muhongo alisema kuwa serikali imedhamilia kukamilisha umeme katika vijiji vyote na visiwa ifikapo mwaka 2021 na kuwa umeme huo wa REA gharama yake ni chini zaidi. 

Hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali kwani ina nia nzuri ya kuwasaidia wananchi wake. 

"suala hili la umeme linafanyika kwa faida ya wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama hivyo ni matumaini yangu hakuna mbunge atakayekwamisha bajeti "

Aidha waziri huyo alisema kuna baadhi ya watanzania wanadai hawaoni faida ya gesi ila ukweli gesi inawanufaisha watanzania wote kwani umeme huo wanaoupata sehemu kubwa gesi inahusika. 

Kuhusu wakandarasi wanaotekeleza mradi huo aliwataka kuifanya kazi hiyo kwa uadilifu na kuwa kampuni itakayozembea itaondolewa. 

Pia aliagiza wenyeji wa maeneo mradi huo unafanywa kuhakikisha wanapewa kipaumbele kupewa kazi na kuwataka wanaopewa kazi kuwa waaninifu. 

Wakati huo huo waziri Prof Muhongo amepongeza kazi kubwa inayofanywa na mbunge wa Kilolo Bw.Mwamoto kuwa muda Mwingi bungeni amekuwa akipigania wananchi wake wapate umeme na ndio sababu ya mradi huo kimkoa kuzinduliwa jimboni Keane. 

Pamoja na pongezi hizo bado aliwaomba wananchi wa kilolo kuendelea kufanya kazi na Mbunge huyo na ikiwezekana mwaka 2020 kupitishwa bila kupingwa. 

"Nimekupenda Sana mbunge Mwamoto unafanya kazi nzuri bungeni na jimboni mimi zawadi yangu kwako nitakupatia vitabu vya kutosha vya masomo ya Sayansi kwa ajili ya shule ya sekondari hii iliyoimba hapa leo"

Kwa upande wake mbunge Mwamoto alimshukuru waziri huyo na kuwa kati ya mawaziri wachapakazi Prof Muhongo ni mmoja wapo na kwa upande wake atakuwa wa kwanza kuikubali bajeti yake na ile ya waziri wa fedha. 

Awali akimkaribisha waziri huyo mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliomba mradi huo kupita maeneo yote ya taasisi. 

Taarifa nzima ya mkuu wa mkoa wa Iringa itakujia hivi punde hapa

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE