March 2, 2017

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA KAMATI INAYOSGHULIKIA MGOGORO WA LOLIONDO


GAM1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia)leo 2 February 2017 amepokea  Taarifa ya Kamati inayoshughulikia Mgogoro wa  Loliondo Kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  amabye ni  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo, Wanao shuhudia  Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania  Martine  Loiboki, Mkuu wa Wilaya ya Loliondo Rashid Taka, Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Wanyama Pori  Prof Alexander  Songorwa, Mkurugenzi Mkuu wa Thomson Safari s John Bearcroft , Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Milian Ole Nasha (MB) ,Mwenyekiti wa CCM Arusha  Lekule Laiser  , Mkurugenzi wa Baraza la Wafugaji Wanawake Bibi Maanda Ngoitika , Kikao hicho cha Kukabidhi Tarifa kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma
Picha na PMO
GAM2 GAM3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia)leo 2 February 2017 akionyesha Kitabu cha Taarifa ya Kamati inayoshughulikia Mgogoro wa  Loliondo Kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  amabye ni  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo, Wanao shuhudia  Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania  Martine  Loiboki, Mkuu wa Wilaya ya Loliondo Rashid Taka, Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Wanyama Pori  Prof Alexander  Songorwa, Mkurugenzi Mkuu wa Thomson Safari s John Bearcroft , Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Milian Ole Nasha (MB) ,Mwenyekiti wa CCM Arusha  Lekule Laiser  , Mkurugenzi wa Baraza la Wafugaji Wanawake Bibi Maanda Ngoitika , Kikao hicho cha Kukabidhi Tarifa kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma
Picha na PMO
GAM4
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisikiliza Tarifa ya Mgogoro  wa  Loliondo  kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati na Mkuu wa Mkoa  wa Arusha , Bwana Mrisho Gambo.
GAM5
Waziri Mkuu Kassi Majaliwa akiwa katika kikao cha Wanakamati wanaoshugulikia Mgogoro wa Loliondo Kikao hicho kimefanyika katika  Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma
Picha na PMO
………………………………………………………………..
*Tumedhamiria kumaliza migogoro nchini
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya Kamati Teule ya Kushughulikia Mgogoro wa Loliondo na kuahidi kuifanyia kazi pamoja na mawaziri husika.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Machi 2, 2017) katika kikao alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma ili kupokea taarifa ya Kamati Teule ya Kushughulikia Mgogoro wa Loliondo. Aliiunda Kamati hiyo, Desemba mwaka jana, mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Kiini cha mgogoro huo ni eneo la pori tengefu la Loliondo ambalo linagombewa na wawekezaji, wakulima, wawindaji kwa sababu ni mapitio ya wanyama, chanzo cha maji, mazalia ya wanyama, malisho ya mifugo na makazi.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza migogoro yote inayowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ukiwemo wa Loliondo uliodumu kwa miaka 25.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo ilikuwa na jukumu la kufanya mapitio ya nini kinachosababisha kuwepo kwa migongano katika eneo hilo ili Serikali itoe uamuzi wenye tija.
“Hatuwezi kuwa tunagombana miaka na miaka bila ya kuwa na solution, hilo hatuwezi kuendelea nalo lazima tushirikiane kumaliza migogoro. Nataka nchi nzima iwe na amani na utulivu,“ amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza migogoro hiyo ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea kushiriki shughuli nyingine za maendeleo.
“Wananchi ndio tegemeo letu na tunataka kuona wakinufaika na Serikali yao.Na Serikali haiko tayari kuona migogoro hiyo ikiendelea. Natumaini timu hii itatuwezesha kumaliza mgogoro huu,“ amesema.
Pia Waziri Mkuu amewataka wadau wote katika maeneo mbalimbali nchini wahakikishe wanadumisha amani na washirikiane vizuri na Serikali na inapotokea dosari wasiingize ushabiki usiokuwa na tija.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza Maofisa Mifugo katika halmashauri zote nchini wahakikishe wanashiriki shughuli za wafugaji ili kujua idadi ya mifugo na changamoto zinazowakabili.
Waziri Mkuu amewataka Maofisa mifugo wawasimamie shughuli za wananchi husasan wafugaji kwa kuonyesha mahitaji ya mifugo iliyoko katika maeneo yao na kuyafanyia kazi.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo Bw. Gambo alisema mgogoro huo ulioanza mwaka 1992 ulikuzwa na makundi mbalimbali kutokana na manufaa yao binafsi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE