March 19, 2017

WAZIRI MKUU AMUWALIKISHA RAIS UZINDIZI WA JUKWAA LA UCHUMI AFRIKA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi
19, 2017) kwa ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli
katika mkutano wa kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam Waziri
Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Mheshimiwa Vishnu
Lutchmeenaraidoo.
Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo
utawakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara
pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.
Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na
mkewe Mama Mary Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la
Biashara kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017.
Aidha, Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea
maeneo maalumu ya uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo.
Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Viwanda na
Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa
Serikali.
*IMETOLEWA NA:*
*OFISI YA WAZIRI MKUU,*
*JUMAPILI, MACHI 19, 2017.*

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE