March 14, 2017

WASIFU WA MAREHEMU BALOZI SIR CLEMENT GEORGE KAHAMA

kahama+pic
Balozi Clement George Kahama, aliyejulikana zaidi kama Sir George alizaliwa tarehe 30 Novemba, 1929 katika Wilaya ya Karagwe na kufariki dunia tarehe12 Marchi, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa Figo Renal Failure)  kwa takribani miaka miwili.
Katika uhai wake, Marehemu alifanyakazi katika Serikali kwa vipindi mbalimbali zaidi ya miaka 50 ikiwemo awamu tatu za uongozi wa taifa hili baada ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961. Marehemu Sir George alikuwa miongoni mwa waafrika wachache waliopata fursa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria yaani  Legislative Council mwaka 1957 na miaka miwili baadaye kuteuliwa kuwa Waziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito ya kikoloni kuelekea uhuru kwa nafasi ya Waziri wa Ushirika na Ustawi wa Maendeleo ya Jamii akiwa na Wenzake wazalendo Chief Abdalah Fundikira, Amir Jamal, na Solomon Eliufoo na Mwalimu akawa Waziri Kiongozi ( Chief Minister).
Baada ya Uhuru Mwaka 1961, Mhe Balozi George Kahama aliteuliwa kuwa Waziri wa kwanza wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Baraza la Mawaziri la Watu tisa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru.Kutoka Uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 2005 Sir George Kahama aliuteuliwa na Baba wa taifa na baadaye Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, kushika nyazifa za Wizara mbalimbali serikalini zikiwemo Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, Wizara ya Biashara na Viwanda, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ushirika na Masoko, Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma na wakati huo  huo akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).
Katika muda wote wa utumishi wa Umma, Sir George aliaminiwa sana na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere baadaye Mhe Benjamin Mkapa kwa nyakati tofauti waliweza kumtuma katika nchi mbalimbali kuwa wakilisha kama mwakilishi maalum wa Rais (Special Envoy) katika nchi mbalimbali ikiwemo Zaire ambayo sasa  inajulikana kama DRC, Burundi na Rwanda,  Holy See (Vatican) na nchi nyingine.
Kazi nyingine alizowahi kufanya Mhe Sir George Kahama ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Maendeleo la taifa (NDC),taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia uanzishwaji wa Viwanda nchini, Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa Kituo  cha Kuvutia wawekezaji (IPC) ambacho baadaye kimekuja kujulikana kama  Tanzania Investment Centre-TIC. Kablaya Uhuru Sir George alikuwa kiongozi wa Chama cha ushirika cha Bukoba, chama ambacho kilitoa msaada mkubwa wa hali na mali katika kusaidia harakati za ukombozi na kuimarisha TANU kama ilivyokuwa kwa vyama vingine vya Ushirika katika maenembalimbal nchini. Itakumbukwa kuwa Wazalendo watano waliounda Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito mwaka 1959 akiwemo Mzee Paul Bomani, Chief Abdullah Fundikira (Tabora), Solmon Eliufoo (Kilimanjaro), Amir Jamal ( Morogoro) na Kahama Mwenyewe (Kagera) walikuwa viongozi katika vyama vya ushirika katika maeneo waliyotoka.
Aidha, katikaUhai wake, Sir George Kahama aliwahi kutumikia taifa katika  nyanja za kidiplomasia kama Balozi wa Tanzania Ujerumani mwaka 1965-1966, Baloziwa Tanzania China (1984- 1989) na Balozi wa Tanzania Zimbabwe (1989-1991).
Katikauhai wake, Sir George KahamaaliwahikutunikiwanishanimbalimbalizakitaifanaKimataifaikiwemo Knight Commander of the Order of St. Gregory the Great iliyotolewana Pope John XXIIImwaka 1962. Hiindiyonishaniiliyozaajina la Sir George.Nishanizinginenikama“The Order of Kilimanjaro iliyotolewanaRaisMstaafu Ali Hassan Mwinyi 1990,ambayoninishaniyajuukabisawanayotunukiwawatumishiwaumma. Mwaka 1975-1976 alikuwaMjumbewaKundi la WatuMashuhuridunianiwalioteuliwanaKatibuMkuuwaUmojawaMataifakufanyautafitikuhusuatharizaUendeshajiwaMakampuniMakubwayaKimataifakatikauchumiwanchizanazoendelea.
Mabadilikombalimbaliyaliyofanyikandaniya Chama cha MapinduzinaSerikaliikiwemoSerikalikuhamia Dodomakwakasikubwanachamakuimarikazaidikumetokeasikuchachekablayakufarikikwakenakutimizandotoyakezaidiyamiaka 40 aliyojishughulishanamradiwaUstawishajiyaMakaoMakuu.
Mwaka1976, Sir George aliteuliwanaSerikaliya Nigeria kamaMjumbewaKamatiyawatuwatatuwaliopewakaziyakufanyatathminiyamchakatowauhamishajiwaMjiMkuuwa Nigeria kutoka Lagos kwenda Abuja.
Sir George aliwahikuandikamaandikonavitabumbalimbalikatika Nyanja zaKidiplomasia,  Ushirika, Uchumi,  MaendeleoyaUjenzi,ikiwemokitabu cha “The Challenge for Tanzania’s Economy” kilichochapishwanakampuniya JamesCurrey Heinemann yaUingelezana “Tanzania into the 21stCentury”,piaalichangiakuandikakitabu cha “The First Tanganyika Industrial Development Blue Print” pamojana  Arthur D. Little Inc. waMarekani.
MbalinautumishiSerikalini, Sir GeorgeKahamaalikuwa Baba mzuriwafamiliaaliyependaumojawafamilianaalikuwa baba tuliyemtegemeakwaushaurinadirakatikamaishayetu.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe
UtaratibuwaMaombolezonaMazishiyaBalozi Sir Clement George KahamaaliyefarikiDuniatarehe 12 Machi, 2017
Mwiliwamarehemuutawasilinyumbanikwakeeneo la Mikocheni B kituo cha Mabasikijulikanachokama Business, mnamosaa 11 jionitarehe 15 Machi, 2017 (Jumatano) nakukeshahadiasubuhitarehe 16 Machi, 2017.
MwiliwaMarehemuutaondolewanyumbanikwakekuelekea Julius Nyerere International Convention Centre kuanziasaambilikamilikwaajiliyaviongozimbalimbalinawananchikutoaheshimazaozamwishokablayakuelekeaKanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saatanonanusu 5.30 asubuhikwaibada.
IbadayamazishiitafanyikakatikaMakaburiyaKinondonikuanziasaatisananusu  9.30 alasili.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE