March 9, 2017

WAPINZANI WA YANGA CAF KUTUA LEO

Zanaco_Team_Picture
Na.Alex Mathias
Timu ya Zanaco FC toka Zambia ambao ni wapinzani wa Yanga katika Michuano ya Klabu bingwa barani Afrika wanatarajia kuwasili leo kwenye ardhi ya Tanzania Majira ya saa kumi jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa Shirika la Ndege la Rwanda.
Zanaco FC ambao Jumamosi ya wiki hii watashuka dimbani kucheza na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania nafasi ya kutinga hatua ya Makundi.
Mabingwa watetezi hao wa Zambia hii itakuwa mara ya pili kukutana na Yanga katika mashindano ya CAF kwani walikuja mwaka 2006 ambapo waliweza kuwang’oa Yanga kwa jumla ya magoli 3-2,Mchezo wa kwanza ulichezwa Dar es salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 na ilipoenda enda Zambia Yanga walifungwa 2-0 na Zanaco kusonga mbele kwa jumla ya magoli 3-2.
Yanga itaingia uwanjani kwa lengo la kulipa kisasi huku ikiwa na morali ya kuwa na kocha Mzambia ambaye anaifahamu vyema Zanaco kwani Msimu uliopita alikuwa anakinoa kikosi cha Zesco United ambao walifika nusu Fainali ya Michuano klabu bingwa Afrika.
Zanaco FC wamekuwa wasili kusema kuwa watawasili lini ila uchunguzi uliofanywa na mtandao wa FULLSHANGWEBLOG kuwa timu hiyo itawasili Leo majira ya saa kumi na dakika tano tayari kwa mtanange huo wa Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE