March 21, 2017

WANANCHI NYANZWA KILOLO WAPONGEZA ASASI YA MMADEA KWA KUWAPATIA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO


Mkurugenzi mtendaji wa MMADEA Raphael Mtitu akipokea pongezi za wananchi wa Nyanzwa 
...................................................
WANANCHi wa kataya Nyanzwa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wamepongeza asasi yaisiyo ya kiserikali ya mahenge mazombe devolopment association(MMADEA) kwa kusaidia kuelimisha wananchi kuendelea nautamaduni wao wa kuoa wadodo wadogo pamoja na afya ya uzazi kwa mama na mtoto.

Wakizungumza namwandishi wa habari hizi wakati wa mikutano ya tathiminiya mradi shughuli za MMADEA zilizofanyika katika kata hiyojana wananchi hao walisema kuwa awali wananchi katika kata hiyo ilikuwa ni utamaduni wao kwawatu wazima kuoa watoto chini ya miaka 18 ila baada ya kupewa elimu hiyo na MMADEA kwa sasahakuna ndoa za utotoni zinazofungwa wala hakuna mwananchianayejihusisha na mahusiano ya mtoto .

Abdalah Juma mkazi wa kijiji cha Nyanzwaalisema kuwa idadi ya wananchi kuendelea na mahusianona watoto wadogo katika kijiji hicho imepungua baada ya elimu ya mara kwamara iliyotolewa na asiasi hiyo ya MMADEA na hivyo kwa sasa jamii imekuwa na lengo moja la kulinda watoto hao .Hivyo aliomba serikali na asasi hiyo yaMMADEA kuendelea kutoa elimu hiyo mara kwa mara na katika maeneo mengine ya mkoa wa Iringa kwani mbali yakijiji na kata hiyo ya Nyanzwa yapo maeneo ambayo hayajafikiwana elimu hiyo .
Akizungumza kwa niaba ya wanawake wenzake Neema Nzakule (19) alisema kuwa aliolewa akiwa na miaka14 na sasa ana watoto watano na awali alikuwa hakuwa na elimu yeyote juu ya afya ya mama na mtoto ila baada ya kushirikiwarsha mbali mbali ambazo MMADEA wamekuwa wakizitoa katika kijiji chao amekuwani mshiriki mzuri wa kuhudhuria kliniki pamoja na kuwaelimisha wanzake kuepuka ndoa za utotoni .


"Mimi ni mmoja kati ya wanufaika wakubwa wa mafunzo mbali mbaliambayo yamekuwa yakitolewa na shirika la MMADEA na kila napo sikia wanakuja huwa nasitisha shughuli zangu zote ili kushirikimafunzo yao maana na yamenisaidia sana nimeweza kuboreshaafya yangu "


Alisema kuwa alilazimishwa na wazazi wake kuolewa na mwanaume mwenye miaka zaidi ya 40 kutokana na kuwa na pesa na ng'ombe nyingina alipotaka kukataa alitishwa ila alivumilia na kwa sasakupitia elimu ambayoanapatiwa ameweza kumfanya mwenziwake huyo kuhudhuria kliniki pamoja .

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyanzwa Samsoni Sambuli alisema kuwa kupitia elimu inayotolewa na MMADEA kijiji kimeweza kuwa na mabadiliko makubwa na hata kujiwekea sheria ndogo ya kuwalea watoto wadogo kwa kuwawajibisha wanaume wanaojihusisha na mapenzi na watoto .

 Alisema kwa kijana au mwanamke atakayekutwa katika mazingira tata na mwanafunzi adhabu yake ni kutozwa faini isiyo pungua shilingi 30000 ama kufikishwa mahakamani na kuwa wapo waliokutwa na adhabu hiyo.


Muuguzi mkuu wilaya ya Kilolo Withnes Mlowe alisema kuwa kasi ya mimba zautotoni kwenye kata hiyo imepungua sana na kuwa suala la afya ya mama na mtoto limepewa kipaumbele huku akitakawananchi kurejesha utamaduni wa unyagokwa vijana wao ili kuwapa elimu ya uzazi mapema.

“ unyago naotaka sio wa ukeketaji niule wa kuwapa elimu juu ya afya zaoili kuwaepusha na majanga mbali mbali “

Mkurungezi wa MMADEA Raphaeli alisema maradi huo unafanyika kwenye kata tatu ya Nyazwa Ibumu Idete .

Mkurugenzi wa MMADEA Bw Mtitu akiahoji walimu wa Shule ya msingi Igunda juu ya mrejesho wa mafunzi waliyopewa juu ya afya ya mama na mtoto 
mwezeshaji Wa MMADEA Winfrida akitoa elimu ya afya ya mama na mtoto kwa wananchi wa Igunda

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE