March 3, 2017

WANANCHI IRINGA WAOMBWA KUSHIRIKI VITA YA POMBE YA VIROBA

RC  Iringa Amina Masenza  akizungumza na  wanahabari  leo ofisini kwake juu ya pombe ya  Viroba
Wanahabari Iringa  wakimsikiliza mkuu wa mkoa
 
Na MatukiodaimaBlog 
MKOA  wa  Iringa umewataka wananchi na  viongozi wa  serikali za  vijiji na mitaa pamoja na  wakuu  wa  wilaya  zote tatu za mkoa  huo kusaidia   kutekeleza agiza la waziri agizo la  waziri  mkuu wa jamahuri ya  muungano wa  Tanzania Kassim Majaliwa  kwa  kuwafichua  wauzaji  na  watumiaji wa  pombe kali ya  viroba iliyofungashwa katika mifuko ya  Plastini.

Imeelezwa  kuwa tamko la  waziri  mkuu la  kusitisha utumiaji ,uuzaji na  ufungashaji wa  pombe kali  kwenye mifuko ya Plastiki  maarufu kama  viroba  lililotolewa Februari 16  mwaka  huu utekelezaji   wa maelekezo ya  tamko  hilo la  waziri mkuu umeanza toka   Machi mosi mwaka huu  hivyo tayari mkoa  umeanza oparesheni  kali ya  kuwasaka wale  wote wanaokiuka agizo hilo.

Akizungumza na  wanahaabari leo   ofisini kwake  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema kuwa agizo  hilo  limekuja  kufuatia athari kubwa hasa kwa vijana na baadhi ya  watoto wanaotumia  pombe   hiyo na kutokana na matumizi  makubwa ya  pombe  hiyo ambayo huuzwa bei ya chini na ubebaji wake ni mwepesi  kwa  watoto wa shule na  waendesha  boda boda  serikali  imeamua  kuzuia uuzaji na  utumiaji wa pombe hiyo iliyopo kwenye  Viroba .

  Huku  akikwepa  kuyahusisha  matukio yote ya ajali za  boda boda kama  yanasababishwa na watumiaji wa pombe  hiyo  ila alisema baadhi yao  wamekuwa wakipata ajali  kutokana na matumizi ya  viroba na  wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto huku  wakiwa  wanakunywa viroba  kutokana na pombe   hiyo  ni rahisi  zaidi kuiweka  mdomoni  huku wakiwa  wanaendesha  vyombo   hivyo  vya  moto na kwa  baadhi ya  wanafunzi  huingia na  pombe   hiyo  darasani bila  walimu  kuwaona.

Alisema  kutokana na madhara na  utekelezaji wa agizo la  serikali  mkoa  wa Iringa umetoa maelekezo kwa  wakuu wa wilaya  kwa  kushirikiana na kamati za  ulinzi na usalama  za wilaya  kufanya  oparesheni  ya  kudhibiti matumizi  ya  Viroba  katika maeneo yao .

" Pombe kali za  viroba  zitasakwa  kuanzia  kwa wasambazaji ,wanunuzi ,wauzaji wote watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali  za  kisheria ...aidha  kwenye  vijiji kamati  za  ulinzi za  vijiji au miotaa nazo zimeelekezwa  kufanya oparesheni  ya kuthibiti matumizi ya  viroba  hivyo  nawaomba wananchi  wote  kutoa ushirikiano katika  kufanikisha udhibiti wa viroba ... Viroba ni  pombe  kama  konyagi hivyo serikali haijapiga marufuku matumizi ya konyagi za chupa ila  imezuia pombe  hiyo  iliyopo kwenye mifuko ya plastiki na  pombe  iliyopo  kwenye  chupa  ni vigumu mwendesha   boda boda  kuitumia huku  akiendesha usafiri huo ama mwanafunzi kuingia nayo darasani bila  kuonekana"


Kuhusu vita  dhidi ya dawa ya  kulevya  ndani ya  mkoa  alisema  mkoa  umefanikiwa  kuwakamata   watumiaji na  wauzaji  wa dawa za  kulevya  15  kati yao  wanawake ni  wawili  ambao  watafikishwa mahakamani  baada ya  upelelezi wao  kukamilika  huku  akidai kuwa  baadhi ya  wafanyabiashara  wa  dawa  za  kulevya  waliotajwa  kuhusika na mtandao wa uuzaji wa dawa   hizo  wamekimbia mkoa na  jitihada za  kuwasaka zinaendelea.

Pia  aliwataka   wananchi  wa mkoa  wa Iringa  kuendelea  na vita ya  kuwafichua   wale  wote wanaojihusisha na  matukio ya  ubakaji  na  kuwafichua ili  kufikishwa  mbele ya  sheria.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE