March 9, 2017

WAAJIRI WOTE TANZANIA BARA KUWASILISHA TAARIFA YA MAPATO YA MWAKA YA WAFANYAKAZI WAO

wcf
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) anawataarifu waajiri wote Tanzania Bara kuwasilisha taarifa ya mapato ya wafanyakazi wao (Return of Annual Earnings) kwa kipindi cha mwaka mmoja, yaani kuanzia tarehe 01.03.2016 mpaka tarehe 28.02.2017.
Uwasilishwaji wa taarifa hizo ni kwa mujibu wa vifungu vya 73 (1) na 73 (2) vya sheria ya fidia kwa wafanyakazi sura ya 263 marejeo ya mwaka 2015 kinachomtaka kila mwajiri kuwasilisha taarifa hizo kabla ya tarehe 31 ya mwezi Machi kila mwaka.
Kwa tangazo hili, nawataarifu waajiri wote kuwa uwasilishwaji wa fomu hizo ni kwa kutumia fomu WCR-3 na mwisho wa kuziwasilisha ni tarehe 31.03.2017.
Fomu zilizojazwa kikamilifu ziwasilishwe kwenye ofisi za Mfuko zilizopo ghorofa ya 6, Jengo la GEPF House, Kitalu na 37, Regent Estate, Barabara ya Bagamoyo au Ofisi za Kazi zilizopo mikoani na wilayani Tanzania Bara.
Aidha, fomu WCR-3 inapatikana kwenye tovuti ya Mfuko www.wcf.go.tz, Makao Makuu ya Mfuko au kwenye Ofisi za Kazi zilizopo mikoani na wilayani Tanzania Bara. Kwa mawasiliano zaidi piga simu za bure 0800110028 au 0800110029.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)

Kitalu na. 37, GEPF House, Barabara ya Bagamoyo, Regent Estate, Ghorofa ya 6.
S.L.P 79655,
Simu: +255 22 2926107, +255 22 2926108,
Nukushi: +255 22 2926109,
Barua pepe: info@wcf.go.tz,
Bovuti: www.wcf.go.tz,
DAR ES SALAAM.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE