March 13, 2017

VIONGOZI WA SIASA MUFINDI WAONYWA KUINGIZA SIASA MRADI WA MAJI WA RDO

VIONGOZI na wanasiasa katika kata ya Mdabulo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wameonywa kuingiza siasa katika mradi wa maji uliofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni 200 na shiriki lisilo la Kiserikali la Rural Development Organization (RDO)

Onyo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati akifungua mradi huo kwenye kijiji cha Ikanga juzi.
Alisema kuwa lengo la wafadhili wa RDO kusaidia mradi huo ni kutaka kunusuru wananchi ambao walikuwa wakitabika na ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa muda mrefu hivyo hatapenda kusikia ama kuona wanasiasa wanavuruga mradi huo kama walivyoanza kufanya hivyo awali .

Kuwa ofisi yake itawachukulia hatua kali wote ambao watabainika kuugeuza mradi huo kuwa ni mradi wa kisiasa ama kuhujumu miundo mbinu ya mradi huo .
" Nawapongeza sana wadau wetu wa maendeleo wilaya ya Mufindi RDO kwa kusaidia mradi huu wa maji ni mradi mzuri uliotumia fedha nyingi hivyo sipendi kuona siasa inaingizwa katika mradi huu naomba nipeni taarifa kwa yeyote atakayeingiza siasa ili nimshughulikie .......na naagiza utaratibu wa uendeshaji wa mardi ufuatwe ikiwa ni pamoja na wananchi kuchangia mradi huo"

Hata hivyo alisema jitihada zinazofanywa na RDO katika wilaya ya Mufindi na Kilolo ni kubwa na serikali inatambua mchango huo mkubwa wa kusaidia huduma ya maji pia kusaidia kutoa elimu kwa watoto yatima.

Mratibu wa RDO Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umekabidhiwa kwa jumuiya ya watumia maji inayojumuisha vijiji vilivyopo katika kata yamdabulo (Kidete, Ludilo na Ikanga) yenye usajili namba 007 na kuwa shirika la RDO tayari linausajili namba 00NGO/00007700 na ndio walezi wakuu wa miradi hiyo ya maji.

Kuwa RDOMdabulo ikisaidiana na nguvu ya wananchi tangu mwaka 2013 kwa lengo la kutatua changamoto za maji katika kata ya Mdabulo, Ihanu,Ifwagi na Luhunga ikiwalenga hasawatoto yatima, akina mama na jamii nzima inayowazunguka ilianza kazi hiyo ya kutafuta ufumbuzi.

Alisema wanafuaika na mradi huo ni taasisi zaidi ya 7 zikiwemo shule pamoja na watu zaidi ya 1500 na kuwa wamefanikiwa   kujenga tank kuu Ludilo ambalo linapelekamaji ikanga na Kidete , kusafirisha maji kutokakidete mpaka mtaa wa Redi, kutemelea vituo mbalimbalikwa kila kijiji , ili kuweza kujilidhisha maendeleo ya mradi, maabara inayotumikakupimia maji , kila baada ya miezi mitatu, kujisajili katika bonde lamto RUFIJI (Rufiji basin) Wakati changamoto kubwa ni baadhi ya watumiaji maji kutochangia michango,hivyo kumepelekea ugumu wa uendeshaji wa mradi na kubaki kutegemea mlezi wetuambae ni RDO kwa kiasi kikubwa,Siasa kutumika katika mradi, hivyo kumepelekeakuwepo na uchagiaji mgumu wa michango ,viongozi kutowajibika ipasavyo katika kuusimamia mradi wa maji,jamii kupuuzia Elimu wanayopta toka kwa wataalamu hivyo kupelekea mradi kuwa tegemezi.  
Mkurugenzi wa RDO Fidelis Filipatali akizungumza baada ya kuzindua Mradi wa maji
Mkurugenzi wa mradi wa maji wa RDO Fidelis Filipatali akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mwanamke wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Wananchi wakishiriki kusogeza bomba za maji 
Mjumbe wa NEC wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini ambae ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi akisaidiana na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Ikanga mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE