March 8, 2017

UWT IRINGA MJINI YAWAKUMBUKA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA ,WATOA MISAADA MBALI MBALI WAAHIDI KUSAIDIA BWENI LA WANAWAKE WALIOATHIRIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Mkurugenzi wa  kituo cha waathirika  wa dawa za kulevya  Dkt  Ally  Ngala  akipokea  misaada  toka  kwa  wanawake  waliotembelea  kituo  chake eneo la Ngome  Iringa
USIKOSE VIDEO YA  TUKIO HILO LOTEUMOJA wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT)  mkoa wa Iringa umefanya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kuwatembelea vijana walioathirika na dawa za kulevya waliopo kituo cha Iringa Sober House kutoa msaada.

Kuwa kuwasaidia vijana hao walioathirika kwa matumizi ya dawa za kulevya ni jambo la msingi na kuwataka wanawake kuwa mbele kupiga vita vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya. 


Akiwashukuru UWT mkoa wa Iringa mara baada ya kushiriki kufanya usafi soko kuu la Manispaa ya Iringa leo kabla ya kwenda kutoa msaada huo, mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema Wanawake hao wameonyesha mfano mwema kwa jamii .


Hata  hivyo  umoja   huo  wa wanawake   Iringa mjini  umeahidi  kutoa  ushirkiano kwa  uongozi  wa  kituo cha  waathirika  wa dawa za kulevya  mjini Iringa  ikiwa ni pamoja nakusaidia  ujenzi wa bweni  la  wanawake walioathirika na dawa  za  kulevya .


Ahadi  ya  kusaidia  ujenzi  wa bweni  hilo ilitolewa na mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Iringa  Ritta Kabati ambae  aliongozana na  wanawake hao pamoja na viongozi  mbali mbali  wa   CCM mkoa  akiwemo mwenyekiti wa CCM mkoa na katibu wa UWT mkoa  wakati akitoa  salam  zake .


Katibu  wa UWT  wilaya ya  Iringa mjini Cecilia Ismail alisema  kuwa wameamua  kuadhimisha siku  ya  wanawake  kwa kuwasaidia  watu  hao  ambao wameathirika na dawa za  kulevya kama  njia ya  kuiunga mkono  serikali ya chama cha mapinduzi  katika  vita ya dawa  za kuevya  nchini.


Alisema  kuwa  wanawake katika Manispaa ya  Iringa  pamoja na kufanya  usafi soko  kuu la Manispaa ya  Iringa  wamefika  kituoni hapo  kutoa msaada wa chakula  na vitu mbali mbali kwa ajili ya mahitaji ya  waathirika  hao  na kuomba  jamii  kuzidi kusaidia  vijana  kujiepusha na dawa za kulevya 
  
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE